Picha ya juu, Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akiangalia zao la mananasi lilivyostawi, katika shamba la SISIMUA Estate, lililopo Kwamsisi. Picha inayofuata ni migomba wakati ya chini ni DC akimuangalia mbwa katika shamba hilo.
MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo
Rweyemamu, amesema kwamba kuna haja ya wananchi wa Handeni kuwekeza zaidi
kwenye kilimo badala ya kuwaachia wageni au matajiri na kuwaachia ardhi zao kwa
bei ya kutupwa.
Muhingo aliyesema hayo juzi
alipotembelea shamba la SISIMUA Estate, lililopo katika kijiji cha Kwamsisi, akiwa
na baadhi ya wanafunzi kutoka shule za Kwamsisi, Kwalugulu na Handeni Mjini, katika
lengo la kujifunza masuala ya kilimo cha kisasa.
Akizungumza na Handeni Kwetu,
Muhingo alisema kilimo ndio uti wa mgongo, hivyo watu wajiingize humo kwa ajili
ya kujitafutia maisha yao, badala ya kuuza ardhi zao kwa bei ya kutupwa, wakati
wangeweza kujiendeleza kimaisha.
“Huu sio muda wa kuacha kulima na
kuwaachia wawekezaji ambao kwa kiasi kikubwa sisi tunakuwa hatuna cha kufanya,
hivyo nadhani Watanzania wote pamoja na watu wa wilaya yangu tungezinduka sasa.
“Naamini tukifanya hivyo, mambo
yatakuwa mazuri ukizingatia kwamba tuna ardhi kubwa na yenye rutuba, ndio maana
wageni wanakuja kwa wingi kwa nia ya kuwauzia mashamba wakati tunaweza kulima
wenyewe na kuinua maisha yetu,” alisema Muhingo.
Muhingo aliitumia siku ya Jumamosi
ya Desemba 8 kuzunguukia katika vijiji mbalimbali vya Kwamsisi kwa nia ya
kuangalia changamoto za wananchi, ikiwamo elimu na kilimo, haswa kwa kutembelea
pia shamba la kisasa.
No comments:
Post a Comment