Na Mwandishi Maalum
MSANII wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael, maarufu kama 'Lulu', kesi yake ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, imezidi kupigwa kalenda kwa madai upelelezi wake haujakamilika.
Lulu Michael, Lulu
Kwa sababu hiyo, kesi ya msanii huyo iliahirishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu
Mkazi, Augustino
Mbando.
“Mheshimiwa hakimu, upelelezi
wa kesi hii haujakamilika, tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa,” alidai Wakili
wa Serikali, Kenneth Sekwao.
Hakimu Mbando alikubali
kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 17 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.
Mshitakiwa anatetewa na
mawakili, Kennedy Fungamtama, Peter Kibatara na Fulgence Masawe.
Lulu yuko rumande kwa miezi
nane sasa kutokana na makosa ya mauaji na kukosa dhamana, anadaiwa kwamba
Aprili 7 mwaka huu maeneo ya Vatican ,
Sinza, alimuua Steven Kanumba.
Kuchelewa kukamilika kwa
upelelezi kumeanza kuzua mjadala kwa watu mbalimbali wanaofika kusikiliza kesi
hiyo, wakidai kwamba hawajui matukio gani nchini ambayo upelelezi wake unaweza
kufanywa kwa haraka.
No comments:
Post a Comment