Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akizungumza na Handeni Kwetu, ofisini kwake
Na Kambi Mbwana, Handeni
MKUU wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amesema kuwa
kamwe hataogopa vitisho wala kutokuungwa mkono katika harakati za kuingoza
wilaya ya Handeni na kufikia malengo aliyojiwekea.
Muhingo aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na Handeni Kwetu, ofisini kwake jana, akielezea mikakati na changamoto anazokutana nazo katika
utendaji wake wa kazi, ukiwamo msimamo wake wa kuhakikisha mabinti wanakwenda
shule.
Akizungumzia suala hilo,
Muhingo alisema kwamba watu wanaodhani kuwa atapunguza makali yake
wanajidanganya, badala yake ataendeleza harakati zake zaidi kwa ajili ya
kuwakomboa kielimu mabinti kutoka kwa wazazi wasiojitambua.
Alisema ingawa zipo changamoto anazokutana nazo, lakini
amekuwa akifanya vikao na kukutana na baadhi ya watu, akiwa na le ngo la
kuwaweka sawa na kuonyesha kuwa nguvu anazotumia hazitapungua zaidi ya
kuziongeza kwa kufanikisha malengo yake.
“Sitapunguza makali bali nitaongeza zaidi hivyo
wanaojidanganya kuwa nguvu hizi zitapungua wanajidanganya, maana lengo hapa ni
kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza wajibu pamoja na wale wazazi wasiowapa
watoto wao nafasi ya kusoma.
“Kazi bado ninayo kubwa sana, hivyo naamini kadri ya uwezo wangu
nitaifanikisha kwa kutetea kile ninachopenda kifanyike na sio kupunguza kasi
yangu, hasa katika suala la elimu ambalo ndio muhimu na mtaji kwa siku za
usoni,” alisema Rweyemamu.
Rweyemamu ni miongoni mwa wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa
hivi karibuni na kuingia kwa kasi sana katika
maeneo yao ya
kazi, huku akisimamia na kuendesha zoezi la kuwakamata wanaowapa mimba au
wazazi wanaowaozesha mabinti zao na kuwaachisha masomo katika sehemu mbalimbali
za Wilaya ya Handeni.
No comments:
Post a Comment