Na Fadhili Athumani, Moshi
07, Desemba
BENDI ya FM academia “Wazee wa Ngwasuma” usiku wa jana
waliuteka mji wa Moshi kwa staili yao mpya ya kucheza ya Vundes katika shoo
kali iliyopigwa katika ukumbi wa Aventure Moshi.
Wakiongozwa na Rais wa Bendi hiyo kongwe katika tasnia ya Muziki wa Dansi hapa nchini Nyosh El Sadaat, vijana hao maarufu kama wazee wa Pamba, walishambulia jukwa la ukumbi huo majira ya nne usiku kwa kuporomosha baadhi ya nyimbo zao za zamani na nyimbo mbili kutoka katika album mpya ya Chuki ya Nini.
Badhi ya nyimbo zilizopigwa katika shoo hiyo ni pamoja na Vuta ni kuvute, iliyo kwenye album ya Vuta nikute, Anna, Maisha Kigeugeu kabla ya kuuteka ukumbi huo uliofurika wapenzi wa muziki wa Dansi kutoka Moshi na Arusha kwa kucheza Staili yao mpya ya Vundes na nyimbo mpya mbili, Maisha uliotungwa na Pablo Maasai na wimbo wa Ndoa ya Kisasa uliotungwa na Mulemule.
Akizungumza na wapenzi wa burudani katika mji wa Moshi, Rais wa Nwasuma, Nyoshi El Sadaat, alisema staili ya Vundes ni moja katika ubunifu waliamua kuja nao kama njia ya kuhakikisha wanaendelea kukaa kileleni katika chati za muziki wa Dansi hapa nchini.
“Vundes ni Ubunifu na moja ya vitu vikali tuliomua kuwaletea nah ii ni kuhakikisha wazee wa Ngwasuma, tunayendelea kuwateka na kuwa nambari wani kwenye muwa dansi, Vundes inamaanisha makalio, ndio maana tunaimba akina dada wanapenda kucheza vundes na akina kaka wanapenda kuangalia vundes, alisema Nyoshi
Bendi hiyo ikidhaminiwa na Windhoek Lager pamopja na SB
Entertainment, leo inaelekea jijini Arusha ambapo kama ilivyokuwa kwa wa Moshi,
watapiga shoo katika ukumbi wa Tripple A, Arusha kwa Kiingilio cha kawaida cha Shilingi 10,000
na VIP ni Shilingi 15000.
No comments:
Post a Comment