Mkuu wa Chuo, Filbert Paschal
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
CHUO
cha The Green Pasture College, kimezimwagia sifa hosteli zao zilizopo kwenye
eneo la chuo chao kuwa ni nzuri na salama kwa wale wanaopenda kusoma na kukaa
hapo hapo.
Jengo la The Green Pasture College linavyoonekana.
Hayo
yalisemwa na Mkuu wa Chuo hicho, Filbert Paschal, alipozungumza na Handeni
Kwetu leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kuanza mwaka wa
masomo.
Akizungumza
zaidi, Paschal alisema kwamba chuo chao kinachotoa pia elimu ya sekondari,
kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, pamoja na elimu ya sekondari kwa miaka
2 (QT), kina hosteli nzuri kwa ajili ya wanafunzi wao.
“Tunaomba
wazazi wawalete watoto wao maana hapa ni sehemu nzuri na hakika inasababisha
mwamko mkubwa wa wanafunzi kusoma zaidi.
“Kila
anayependa kusoma katika chuo chetu akiwa hapa hapa, uwezo huo upo, maana tuna jingo
zuri lenye ubora wa hali ya juu, ikiwa ni njia pia ya kuchangia elimu nzuri.
Mbali
na kutoa elimu ya sekondari, pia The Green College inayopatikana Mwananyamala
Komakoma, inafundisha kozi mbalimbali, ikiwamo ualimu wa chekechekea, masomo ya
biashara, Computer na mengineyo.
No comments:
Post a Comment