Mwimbaji wa Inji, Dorice Mkangama
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa nyimbo wa Injili, Dorice Mkangama ambaye kwa sasa anakamilisha albamu ya tano, amesema kuwa pia yuko mbioni kufyatua filamu sita kwa mpigo ambazo sasa anaendelea kuziandaa.
MWIMBAJI wa nyimbo wa Injili, Dorice Mkangama ambaye kwa sasa anakamilisha albamu ya tano, amesema kuwa pia yuko mbioni kufyatua filamu sita kwa mpigo ambazo sasa anaendelea kuziandaa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, huyo alizitaja filamu
hizo kuwa ni 'Karama ya Almasi', 'Money Kingdom', 'Lango la Giza', 'The Dream',
'The Singer' na 'The Prophetic Sin'.
"Mimi ndiye mtayarishaji na muongozaji huku kazi hii
ikinichukua muda mrefu na sasa niko kwenye hatua za mwisho kukamilisha filamu
hizo," alisema Mkangama na kuendelea:
"Ninamshukuru Mungu kwa sababu amejalia vipaji vingi tu ambavyo ni muhimu nivitumie kwa kazi yake, ndiyo maana ninaimba na pia nina uwezo wa kutunga vitabu," alisema.
Alisema katika kutumia vipaji vyake hivyo, anajiandaa pia
kutoa vitabu
kadhaa vikiwemo vya 'King'amuzi cha Ndoto', 'Miujiza', 'Mjue Adui Yako', 'Upako' na 'Jinsi ya Kujifungua Katika Vifungo'.
kadhaa vikiwemo vya 'King'amuzi cha Ndoto', 'Miujiza', 'Mjue Adui Yako', 'Upako' na 'Jinsi ya Kujifungua Katika Vifungo'.
Alisema kuwa ana kazi kazi tatu ambazo ni za kuandaa filamu,
utunzi wa vitabu na pia kukamilisha albamu mbili kwa mpigo za Namngoja
Bwana na Mvua ya Baraka.
Mkangama alijitosa kwenye muziki wa Injili tangu mwaka 2005
akiwa na albamu ya kwanza ya 'Tazama Bwana' kisha ikafuatia ya pili
iitwayo 'Yesu Namba Moja', 'Mikononi mwa Yesu' na sasa anaandaa mbili kwa
mpigo.
No comments:
Post a Comment