Na Mwandishi Wetu, Kido Jembe
Rais wa Gambia Yahya Jammeh ametoa amri kuwa wafanyikazi wote wa umma
watafanya kazi siku nne pekee kwa wiki kuanzia leo Ijumaa . Ijumaa sasa itakuwa
siku ya mapumziko sawa na Jumamosi na Jumapili.
Rais Jammeh anasema
iwapo wananchi wa Gambia watafanya kazi siku nne kwa wiki watapata muda zaidi
wa kusali, kushiriki maswala ya kijamii na kulima mashamba yao.
Kwenye taarifa
amesema wananchi wa Gambia wanapaswa kurejea mashambani na kupanda chakula na
kuhakikisha wanakula chakula hicho ili taifa hilo liwe tajiri na lenye afya.
Amesema kuwa
mishahara yao haitapunguzwa kwa sababu kwa siku hizo nne watu watafanya kazi
zaidi ya saa za kawaida ili kulipiza siku ya tano.
Shule za kitaifa
hazitafunguliwa tena siku ya ijumaa.Sekta za kibinafsi zitafanya kazi hadi
ijumaa lakini hazitaweza kufanya biashara yoyote na serikali siku hiyo.
Rais Jammeh mwenye
historia ya kuwa na tabia za kustaajabisha, hajawapa wananchi Gambia muda wa
kujiandaa kwa mfumo huo mpya.
Mwaka 2007
alitangaza kuwa anaweza kutibu ungonjwa wa Ukimwi kwa muda wa siku tatu
akitumia mchanganyiko wa dawa za kienyeji. Tamko hilo lililaaniwa na wataalam
wa matibabu kote duniani.
Pia amekuwa
akishtumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadam.
Mwaka jana wafungwa tisa waliokabiliwa na hukumu ya kifo
walipigwa risasi na maafisa wa polisi huku rais Jammeh akiapa kuwaua wafungwa
wote waliohukumiwa kifo katika muda wa wiki kadhaa.
Baadaye alisimamisha mauaji
hayo baada ya kukosolewa vikali na jamii ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment