Kadinali Keith O'Brein
Na Mwandishi Wetu, Scotland
Kardinali O’Brien sasa hatapaswa kusafiri hadi
Vaticana wiki hii, huku taarifa za shutuma zake zikitajwa kufanyika miaka 30
iliyopita.
HALI imezidi kuwa mbaya katika Kanisa
Katoliki duniani, baada ya Padre wake, Kardinali Keith O’Brien wa nchini Scotland, kutangaza
kuachia ngazi katika wadhifa huo mkubwa kulitumikia kanisa lenye waumini wengi
duniani.
Kutokana na hatua hiyo, kiongozi huyo
wa kiroho sasa hatakwenda nchini Italia kushiriki kupatikana Papa mpya, baada
ya yule Benedict XVI naye kujiuzulu na kuifanya nafasi hiyo iwe wazi na kuleta
mtetemko wa aina yake.
Habari kutoka ndani ya Kanisa hilo
zinasema huenda kujiuzulu kwa kiongozi huyo wa kirono zimetokana na baadhi yao
kukumbwa na kashfa ya kuwavunjia heshima makasisi watatu, hivyo kulazimishwa
kuachia ngazi.
Hata hivyo, taarifa hizo zimepingwa na
Kardinali huyo, ingawa upekuzi huo umegundua kuwa kujiuzulu kwa kiongozi huyo ni
kurudisha heshima ya Kanisa Katoliki kutoka hapa lilipokuwa sasa, huku baadhi
yao wakihusishwa kwenye matukio mabaya, yakiwamo yale ya kuwanyanyasa watoto na
waumini wao.
No comments:
Post a Comment