Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Jerryson
Tegete, amesema ingawa timu yao ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0
dhidi ya Azam FC, lakini soka lake na jinsi alivyoshindwa kuifungia mabao timu
yake ameumia na kuona hajajitendea haki.
Bao pekee la Yanga lilifungwa
na Haruna Niyonzima na kupeleka shangwe kwa timu hiyo ambayo kwa sasa
imefikisha pointi 39 na kushika usukani mwa ligi hiyo, ikufuatiwa na Azam FC.
Akizungumza mwishoni mwa wiki
iliyopita, Tegete alisema kwamba alikuwa na nafasi kubwa ya kuifungia timu yake
mabao hata mawili, lakini bahati haikuwa yake.
Alisema jambo hilo limempa
unyonge wa aina yake, akiona kuwa hajaitendea haki Yanga, ingawa walifanikiwa
kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam.
“Nashangaa kwanini nilitoka
uwanjani bila kufunga hata bao moja wakati nilidhamiria na kuipania zaidi mechi
hiyo, ingawa matokeo yake hayakuwa machungu kwakuwa bado sisi tulishinda.
“Matokeo ya kushinda bao 1-0 ni
mazuri kwetu, lakini nilikuwa na uwezo wa kushinda, hivyo nimeumizwa kwakuwa
sijaweza kuingiza bao kimiani na kututoa na ushindi mwembamba,” alisema.
Yanga ipo katika hatua nzuri ya
kuweza kunyakua ubingwa wa Bara msimu huu kwa kuwapoka watani zao wa jadi
Simba, ambayo yenyewe juzi ilishindwa kutoka na ushindi mbele ya Mtibwa Sugar
kwa kukubali kichapo cha bao 1-0.
No comments:
Post a Comment