Mratibu wa Ruaha Marathon, Albert Sanga
Na Rahimu Kambi
SHIRIKA la Mindset Empowerment, waandaaji na waendeshaji wa
mbio za kila mwaka ambazo ni za pili kwa ukubwa Barani Afrika za Ruaha Marathon;
limesema kuwa mwaka huu mbio hizo zimepangwa kufanyika Mei 25, mkoani Iringa.
Mbio hizi zinashirikisha watu wa aina na rika zote wakiwemo
walemavu kwa kukimbia kilomita, 3, 6, 21 na 41.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mratibu wa mbio hizo, Albert
Sanga, alisema kuwa jumla ya washiriki na wageni (2,000) watakuwapo kwenye
mashindano hayo.
Alisema wanatarajia kufanya mashindano yenye mguso kwa mkoa
wao wa Iringa, huku wakiamini pia watu kutoka nje ya nchi watashiriki.
Watu kutoka Mataifa mbalimbali duniani, walihudhuria
mashindano haya mwaka jana, hivyo mwaka huu tunatarajia kupokea washiriki na
wageni wengi zaidi.
"Tumeshaanza kuandikisha washiriki tangu Desemba, 2012,
hivyo natumia fursa hii kuwaalika watu kujiandikisha sasa ili waweze kushiriki
mbio hizi zenye mguso," alisema Sanga.
Aidha waandaaji wa mbio hizo wameweka utaratibu wa
kujiandikisha kwa njia ya mtandao, (online registration) kwa kupitia
www.ruahamarathon.com au kwa namba +255719 127 901.
No comments:
Post a Comment