Ombeni Mbeula akiwa amekaa kitandani ndani ya hospitali ya mkoa wa Dodoma
Huyu ndio mama wa mtoto Ombeni Mbeula anaitwa Kilaudia Kigaila
Huu ndo mwonekano wa mtoto Ombeni Mbeula akiwa amelala hospitalini
Mama wa mtoto Kilaudia Kigaila akiwa na mwanae
Ombeni Mbeula
Nyumba iliungua wakati watoto hao wamekaa ndani na wakati
huo huo mama wa mtoto alikuwa amekwenda shambani maeneo ya Chitemo iliyoko
wilaya ya mpwapwa
Wakati mvua inanyesha ghafla nyumba ilibomoka na wakati
huohuo walikuwa watoto wawili walikuwa jikoni ndani ya hiyo nyumba. Baada ya
tukio hilo kutokea ikafanyika uokoaji kwenye nyumba hiyo maeneo
ya Chitemo na kufanikisha kuokoa watoto
wote wawili kati ya mmoja aliumia kwa kuangukiwa na udongo wa nyumba hiyo na
huyu Ombeni Mbeula aliangukia kwenye moto mpaka kuungua hivi unavyoona kwenye
picha lakin hali zao ni salama kwa wote.
Baada ya uokoaji waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospitali
ya Mima iliyoko Mpwapwa ikashindikana madaktari wakamuagiza aende hospitali ya
Mpwapwa hapo hospitalini wakakaa siku mbili katika hospitali ya mpwapwa na siku ya tatu wakaambiwa waende hospitali
ya rufaa iliyoko Dodoma Mjini ambayo ni inajulikana General kwa matibabu zaidi.
Walipofika katika hospitali ya mkoa wa Dodoma wakaanza
matibabu lakini uwezo wa kipato cha wazazi wake sio kizuri inahitajika msaada
kwa matibabu maana hata dawa hajapatiwa na pesa kwa ajili ya matibabu haikuweza kupatikana paka sasa
Kama umeguswa kutoa ni moyo sio utajiri muokoe mtoto huyu
maana hata kula anashindwa mpaka kuona anaona kwa mbali sana.
Mama yake hana simu lakini anatumia simu ya ndugu yake Ekiria Paskali
Kwa yeyote atakayependa kumchangia mtoto huyo atume chochote
kwenye namba hii au atumie M- pesa kwenye namba hii 0757 498336. PICHA KWA HISANI YA PAMOJAPURE BLOG
No comments:
Post a Comment