Boniface Wambura, Msemaji wa TFF
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja katika viwanja tofauti. Timu hizo zinapambana kutafuta hadhi ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao 2013/2014.
Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa kesho (Februari 23 mwaka
huu) kundi A litakuwa na mechi moja itakayozikutanisha timu za Mkamba Rangers
na JKT Mlale itakayochezwa Uwanja wa Ruaha mkoani Morogoro.
Kundi B lenyewe litakuwa
na mechi mbili; Tessema itacheza na Ashanti United katika Uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume, Dar es Salaam wakati Ndanda itaikaribisha Polisi Dar es Salaam
kwenye Uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara.
Raundi ya 12 ya ligi
hiyo kundi A itashuhudia timu zote nane zikiwa viwanjani; Pamba vs Mwadui (CCM
Kirumba), Polisi Tabora vs Polisi Mara (Ali Hassan Mwinyi), Polisi Dodoma vs
Morani (Jamhuri) na JKT Kanembwa vs Rhino Rangers (Lake Tanganyika).
Jumapili (Februari 24
mwaka huu) kundi A litakuwa na mechi kati ya Burkina Faso dhidi ya Kurugenzi
(Jamhuri), Majimaji vs Polisi Iringa (Majimaji) wakati kundi B ni Transit Camp
vs Villa Squad (Karume), na Green Warriors vs Moro United (Mlandizi).
No comments:
Post a Comment