Mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Perseko Vicent Kone
Na
Salesi Malula, Manyoni
SAKATA la Migogoro ya
Ardhi ambayo imedumu kwa muda mrefu Wilayani Manyoni kutokana na Shinikizo la
Wananchi kuwaondoa Maafisa Ardhi, limefanikiwa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dk.Perseko Vicent Kone kuwasimamisha kazi kwa muda usiojulikana.
Katika
Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mnadani eneo la Majengo
wilayani Manyoni ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida alikuwa katika ziara yake ya
kikazi aliwaruhusu wananchi 45 kutoa kero mbalimbali ambazo zinawakabili.
Mkuu
wa Wilaya Manyoni Bi.Fatma Hassan Toufiq aliwatembelea wananchi wa eneo la
Majengo na Kipondoda na kuombwa kuwatimua Afisa Ardhi Leonard Msafiri, kwakuwa
amekuwa kero kubwa katika wilaya ambapo alikuwa akipora viwanja vya wananchi
pasipo kufuata taratibu wala kuwalipa fidia wananchi wanaomiliki maeneo yao.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida katika ziara yake ya siku tatu wilayani Manyoni akiwa katika
eneo la Majengo na kipondoda aliweza kukutana na madudu ambayo yalikuwa
yakifanywa na Maafisa hao wa ardhi.
Wananchi
45 waliweza kutoa kero zao kuhususiana na kuporwa meneneo yao bila kulipwa
fidia na maafisa wa ardhi ambao walikuwa wakitajwa kwa majina huku baadhi ya
watoa kero wakilia kwa uchungu na kumuomba RC kuingilia kati sakata hilo.
Akijibu
kero zao katika mkutano wa Hadhara DK.Kone alisema amesikia kilio cha wananchi
wa Manyoni na kuanzia sasa
“Ninasimamisha
Shughuli zote za ugawaji na upimaji wa Viwanja wilayani Manyoni mpaka pale
maeneo yote yanayolalamikiwa yawe yamepatiwa ufumbuzi, na nimesimamisha
shughuli zote za ujenzi kwenye maeneo yote yanayolalamimikiwa na kuanzia sasa
nawasimamisha kazi maafisa, Ardhi wanaolalamikiwa Leonard Msafili, John Chima
na Kenedi Chigulu ambao wamesababisha malalamiko haya”.
Huku
akishangiliwa na wananchi alisema “Naunda Tume ya wataalamu watakaotoka Mkoani,
ni tume itakaoshirikisha wataalamu mbalimbali watakaochunguza mgogoro wote na
wanipe mapendekezo, Tume hiyo inatarajia kuanza kazi Februari 4, huku ikifanya
kazi kwa muda wa siku saba kwa kuwahoji wote.
"Nataka
kupitia mgogoro huu wa masuala ya Ardhi kwakuwa ni fundisho kwa watumishi wote
ambao siyo waadilifu na wanaotakiwa wafukuzwe au kupewa onyo.
Aidha
wengine wataburuzwa kortini bila kuonewa haya kwani muda wa kulindana umepitwa
na wakati,” Alisema.
No comments:
Post a Comment