Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi Nchini (IGP) Said Mwema (kulia) Waziri wa Mambo ya ndani Emmanuel
Nchimbi na Kamnda wa Pilisi Zanzibar Ally Mussa kwenye moja ya mikutano na
waandishi wa habari.
SIKU chache baada ya kutokea kifo cha Padri Evarist Gabriel Mushi
kupigwa risasi na watu wasiojulikana kichwani eneo la Beit el Raas, Jana Imamu
wa Msikiti wa Mwakaje ameuawa baada ya kupigwa mapanga hadi kufa.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja,
Ahmada Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hapo jana mchana majira ya
saa 8 na kumtaja aliyefariki kuwa ni Sheikh Ali Khamis ambaye ameuawa na watu
wasiojulikana.
Kamanda Ahmada alisema Sheikh Khamis mbali ya kuwa ni Imamu wa Msikiti lakini
pia ni mkulima na ameuliwa wakati akiwa katika mazingira ya kazi zake ndani ya
shamba lake huko Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akielezea mazingira ya tukio hilo Kamanda Ahmada alisema tukio hilo limetokea
baada ya Sheikh Khamis kwenda shambani kwake katika shmba la minazi Kidoti
ambapo wakati akiwa shambani hapo ndipo walipotokea watu kadhaa na kumpiga
mapanga sehemu za shingoni mwake na kusababisha kifo chake muda mfupi baada ya
kipigo hicho.
Alisema baada ya tukio hilo, watu walimchukua na kumkimbiza hospitali lakini
kutokana na kupoteza damu nyingi alifariki dunia wakati akiwa njiani na hivyo
harakati za mazishi zinafanyika baada ya kuchukuliwa vipimo na wataalamu wa afya.
Kamanda Ahmada ametoa wito kwa wananchi kutopuuzia taarifa za watu ambao
wanawashuku na wenye kuleta maafa yakiwemo mauaji hapa nchini, kwani kuwaficha
wahalifu ni kuendeleza utamaduni usiofaa katika jamii ambayo imeanza kuharibika
kutokana na mauaji hayo yanayoendelea kila kukicha.
Hili ni tukio la nne kwa viongozi wa dini kuhujumiwa ambapo tukio la kwanza
Sheikh Fadhil Suleiman Soraga kumwagiwa tindi kali na watu wasiojulikana na
kujeruhiwa vibaya wakati akifanya mazoezi nyakati za asubuhi karibu na nyumbani
kwake Magomeni, tukio la pili ni lile la Padri Ambrose Mkenda aliyepigwa
mapanga shingoni na kurejuhiwa vibaya na watu wasiojulikana wakati akitaka
kuingia nyumbani kwake huko Tomondo Mjini Unguja. matukio hayo mawili yalitokea
mwaka jana.
Katika mwaka huu nako kumetokea matukio mawili kwa kuuawa kwa Pardi Evarist
Mushi huko Beit El Raas wakati akitaka kuingia Kanisani na pia kuuawa kwa
Sheikh Ali Khamis huko Kidoti shambani kwake Mkoa wa Kaskanizini Unguja. Inna
lillahi wainna ilayhi rajiiun.
|
No comments:
Post a Comment