Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MABINGWA wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC, leo
itamenyana na timu ya Azam FC, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,
ukiwa ndio mchezo unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa kandanda.
Mechi hiyo ya leo, Yanga atakuwa mwenyeji, huku
ukipigwa katika Uwanja wa mpya na wenye kubeba watu wengi, akicheza na timu
inayopanda juu kwa kasi ya aina yake katika soka Barani Afrika.
Timu zote zinabanana kileleni kwa kuwa na pointi 36,
ingawa Azam imecheza mechi moja zaidi, huku zikitofautiana kwa uwiano wa mabao
ya kufunga na kufungwa katika msimamo wan a kila moja ina pointi 36.
Huku timu hizo zikichuana vikali kileleni, lakini pia
vinara wa ufungaji kwenye ligi kwa sasa wanatoka katika timu hizo mbili, Kipre
Tchetche aliyepachika mabao tisa akifuatiwa na Didier Kavumbagu wa Yanga mwenye
mabao nane.
Iwapo timu yoyote itafanikiwa kuondoka na pointi tatu
katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam,
kasi ya mbio za kuwania ubingwa itaongezeka.
Waamuzi wanaotajwa kuchezesha mechi hiyo ni pamoja na
Hamis Chang’walu wa Dar es Salaam na John Kanyenye wa Mbeya, wakati mezani
atakuwepo Oden Mbaga.
Mbali na Yanga na Azam, mechi nyingine zinazopigwa leo
ni pamoja na Mgambo Shooting dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga, wakati Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Polisi Dodoma
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi zote za leo zina upinzani wa aina yake, kutokana
na timu zote kupania kushinda ili zijiweke katika nafasi nzuri, hasa zile
zinazowania ubingwa huo, ikiwamo Yanga, Azam na Simba.
No comments:
Post a Comment