Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.
SERIKALI Serikali kwa kupitia Waziri
wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo,
Dk.Fennella Mukangara, imeingilia
kati na kubadilisha mchakato wote wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),
kwa madai ya kuwa Katiba iliyotumika si
halali.
Habari zilizotufikia Handeni Kwetu leo, jijini Dar es Salaam zinasema kuwa Mukangara aliitaka TFF kufanya
mchakato wao upya kwa kuelekea kwenye uchaguzi huo kwa kuhakikisha kuwa
wanatumia Katiba ya mwaka 2006 na sio mpya iliyozua utata kwa wadau wa michezo
hususan mpira wa miguu.
Waziri huyo alisema kwa kutumia
Ibara ya 10 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuondoa msajili wa
vyama na vilabu michezo. Sakata hilo lilikuja siku chache baada ya Kamati ya
Uchaguzi na ile ya Rufaa ya TFF kuwaengua katika mbio za uchaguzi huo, Jamal
Malinzi na Michael Wambura hivyo kuzua zogo kubwa.
Wiki iliyopita, Serikali kwa
kupitia Waziri huyo wa Michezo, ilifanya kikao cha pamoja na viongozi wa Baraza
la Michezo, akiwa na nia ya kupewa ushauri na kuangalia jinsi mchakato huo
ulivyokwenda hadi kuzua mzozo huo.
Hata hivyo, TFF wao, kwa
kupitia Rais wake, Leodgar Tenga, ilitangaza kusimamisha uchaguzi huo
uliopangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu, kwa madai kuwa utafanyika baada ya
kikao cha wajumbe wa FIFA wanaotarajiwa kufika mapema mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment