DR Shein akihutubia wana CCM katika
Kusheherekea miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Na Mwandishi Wetu,
Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shain amewatoa mashaka wanaohoji kutokuwepo kwa hati halisi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
na kusema hati hiyo ipo na iwapo hawaamini wanaweza kwenda Umoja wa Mataifa New
York.
Amesema
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar chimbuko la kuasisiwa kwake kulitokana na
ridhaa ya wananchi wa pande mbili za Muungano na kuwataka wanaowababisha
wananchi kwa maneno ya mitaani kuacha kufanya hivyo kwa sababu kila swali lao
lina jawabu lake.
Dk
Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyeki wa CCM Zanzibar amesema kuundwa kwa Muungano
halikuwa ni jambo la kubahatisha bali lina malengo yaliokusudiwa kabla ya
kupatikana Uhuru ya Tanganyika mwaka 1961 na kufanyika kwa Mapinduzi matukufu
ya Zanzibar Januri 12,1964
Amesema wenye wasiwasi na kutokuwepo kwa hati ya Muungano wamfuate Ikulu awaonyeshe chumba walichokutana Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume na kufanya makubaliano ya mwisho kabla ya kuunganisha nchi zao.
Amesema wenye wasiwasi na kutokuwepo kwa hati ya Muungano wamfuate Ikulu awaonyeshe chumba walichokutana Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume na kufanya makubaliano ya mwisho kabla ya kuunganisha nchi zao.
Ameeleza
kuwa madhumuni ya vyama vya TANU na ASP yalilingana tokea vyama hivyo vikiwa
katika harakati zake za kujikomboa hivyo kurahisisha hata kazi ya kuziunganisha
nchi hizo mwaka 1964 pia vyama hivyo na kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977.
Aidha
Makamo huyo Mwenyekiti wa CCM amewaeleza wananchi kuwa Mapinduzi ya Zanzibar
ndiyo Uhuru kamili wa visiwa vya Unguja na Pemba huku akiwataka wananchi
kutowasiliza watu wanaopotosha ukweli na kuwataka kuacha kufanya hivyo.
Dk
Shein amesema watu wanaobeza ukweli huo hawana nguvu ya hoja bali wana lengo la
kuwagawa wananchi ili waweze kuyafikia matarajio yao ambayo amesisitiza
yanapaswa kupuuzwa na kila mpenda amani na umoja.
Amewataka
watu hao kupuuzwa kwasababu hawajui wafanyalo na kwamba wanamangamanga ili
kutaka kuwagawa wananchi bila ya kufikiri kwa makini .
Akizungumzia
faida za Muungano Dk Shein amesema kiuhalisia wananchi wa Zanzibar ndiyo
wanaofaidika na Muungano huo kwani kila uendepa katika Tamnzania Bara kuna
wazanaziabri waliotamalaki na kuwekeza miradi na mitaji .
Alisema
Zanzibar inafaidika na siko la Bara ambapo kabla ya Mapinduzi ilikuwa ikiagiza
bidhaa za vyakula na mahitaji mengine kutoka nchi za Pakistan, Japan na
mashariki ya mbali jambo ambalo sasa linapatikana kutoka Mikoa ya Bara.
Kwa
upnde wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizunguimza kabla
ya kumkaribisha Dk Shein ,amesema nguvu ya umoja na maelewano kati ya visiwa
vya Unguja na Pemba inatokana na kuwepo kwa Muungano na kusema nje ya jambo
hilo lolote linaweza kutokea.
Vuai
amesema Muungano wa Tanzania licha ya kuleta tija za kiuchumi lakini pia kwa
kipindi chote cha miaka 49 ya kuwepo kwake umelinda na kusimamia usalama wa
raia na mali zao.
Amesema
hata pale Tanznia ilipovamiwa na majeshi ya Idd Amini mwaka 1978,wanajeshi wa
Zanzibar waliingia vitani ili kuihami nchi yao vikiwemo visiwa vya Unguja na
Pemba na kwamba nje ya Muungano umoja huo unaweza kuparaganyika .
Naibu
huyo Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,amesema CCM itaendelea kujivunia matunda ya
TANU na ASP kutokana na kupigania kwao maslahi ya watu waliokuwa wakikandamizwa
na kubaguliwa katika ardhi ya nchi zao.
Amesema vyama hivyo
kwa pamoja vilihakikiisha vinajenga misingi imara ya heshama na utu kwa kila
binadamu na kuondosha matabaka,ubaguzi wa rangi na maonevu hadi pale vilipoamua
kuunganisha nguvu zake na kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977.
No comments:
Post a Comment