Mkuu wa Wilaya Kilwa, Abdallah Ulega.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HOSPITALI ya Wilaya ya Kilwa imelalamikiwa na wananchi
wilayani humo kwa kukosa dawa, hali inayowapa wakati mgumu wagonjwa
wanaopelekwa hapo kupata matibabu, huku dawa pekee inayopatikana ikiwa ni
Panadol.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao, baadhi ya wananchi wa wilayani Kilwa walisema kuwa kukosekana kwa dawa kwenye
hospitali hiyo kunasababisha watu waishi kwa tabu, huku wengine wakipata
madhara makubwa zaidi.
Alisema mara kwa mara majibu yanayotolewa na viongozi kwenye hospitali hiyo ni
kukosekana kwa dawa, jambo ambalo kwa wananchi wanaotegemea uwepo wa hospitali
ya serikali kunawaweka kwenye wakati mgumu.
Akizungumzia taarifa hizo kwa njia ya simu, Mkuu wa wilaya
wa Kilwa, Abdallah Ulega, alisema matatizo ya dawa kwenye hospitali ya wilaya
yake si habari ngeni, huku akisema kukosekana huko wakati mwingine ni kuchelewa
kufika kwa fedha za kununulia dawa.
Alisema kuwa juhudi zinazofanywa na serikali ya wilaya ni
kufanya mazungumzo na wanaoshughulia na usambazaji wa dawa, ambao ni Bohari Kuu
ya Dawa (MSD), ili kutatua changamoto ya ukosefu wa dawa katika Hospitali hiyo.
“Hospitali nyingi katika baadhi ya wilaya zetu zinaweza
kufikwa na upungufu wa dawa, maana kabla ya kufika, kunakuwa na mizunguuko ya
hapa na pale, ingawa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wake
wanaishi vizuri na kupata matibabu.
“Kwa pamoja tutaliangalia suala hilo na kufanya kazi kwa
nguvu zote kuwahadumia Watanzania, wakiwamo wa wilayani Kilwa kwa kusimamia
vyema na kushauri au kutoa taarifa inapofikia suala la kukosekana kwa dawa za
aina yoyote ile katika hospitali zetu,” alisema.
No comments:
Post a Comment