Francis Cheka (kushoto) akiwa na Adam Tanaka (katikatia) na Thomas Mashali (kulia)
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO
la Ngumi la Kimataifa Afrika (IBF/Africa), limetoa kibali kwa bondia Francis
Cheka ambaye ni bingwa wa Africa katika uzito wa Super Middle kutetea ubingwa
wake dhidi ya bondia Thomas Mashali wa Tanzania, likipangwa kufanyika Mei Mosi,
katika Ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam.
Mabondia
hao wawili walikutana jana Februari 13
katika hoteli ya Ndekha, iliyoko Magomeni Kondoa na kutia sahihi mkataba wa
kupigana kwenye pambano hilo.
Taarifa iliyotumwa na Rais wa Shirikisho
hilo, Onesmo Ngowi, ilisema kuwa Mashali ambaye ndiye bingwa wa Afrika ya
Mashariki na Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle ana kiwango kizuri cha
kushindana na Cheka katika pambalo hilo.
Ilisema kuwa itakuwa mara ya pili kwa
bondia Francis Cheka kutetea mkanda alioushinda Aprili 29, mwaka 2012 dhidi ya
bondia machachari Mada Maugo wa Tanzania.
“Cheka
aliutetea vyema mkanda wa ubingwa wa IBF/Africa dhidi ya bondia Chiotcha
Chimwemwe ambaye ni Afisa katika jeshi la Malawi siku ya Boxing Day (26
Decewmber 2012) katika jiji la Arusha.
“Kama Francis Cheka atashinda tena
pambano hili, atapewa nafasi ya kupigana kugombea mkanda wa IBF wa mabara (IBF
I/C),” ilisema taarifa hiyo.
Pambano hili linaandaliwa na kampuni ya
Mumask Investment and Gebby Pressure ya jijini Dar es Salaam chini ya uratibu
wa Adam Tanaka.
No comments:
Post a Comment