Umemuona jamani Tenga?? Hapa anawaonyesha wanahabari gazeti lilioandika habari za kujiuzulu kwake mwaka 2001....
Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka TFF sasa Shirikisho la Soka nchini
(TFF), Michael Wambura, amesema endapo Tanzania itafungiwa na Shirikisho la
Mpira la Dunia (FIFA), wa kustahili kulaumiwa ni Leodgar Tenga, Rais wa
Shirikisho hilo.
Wambura
alimataka Tenga aitishe mkutano badala ya kufurahia ujio wa viongozi wa
FIFA, ikiwa ni njia ya kutaka Tanzania ifungiwe jambo ambalo likitokea,
Watanzania watalia na Rais huyo aliyemaliza vibaya muda wake wa mwisho.
Aidha,
Wambura aliitaka TFF na Kamati zake zote kuwa ziitishe Uchaguzi Huru,
kabla ya kumaliza muda wake kwa mujibu wa sheria, huku akisema kuwa
uamuzi wa serikali unapaswa kuungwa mkono maana umekuja kumaliza tatizo,
hivyo wanaona kuwa Tanzania itafungiwa basi wa kulia naye ni Tenga.
Baada
ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk.
Fenella Mukangara kutangaza kutoitambua Katiba ya TFF ya mwaka 2012,
Tenga aliitisha kikao cha Kamati ya Utendaji kinachotarajiwa kufanyika
mwisho mwa wiki.
Michael Wambura, akionyesha kipande cha gazeti kwa wanahabari, ambalo mwaka 2001 liliandikwa juu ya kujiuzulu kwa Leodgar Tenga Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), wakati huo ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kama ushahidi wa kigeu geu chake anapokuwa kwenye uongozi.....
No comments:
Post a Comment