Kambi Mbwana, mjumbe
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAKAZI wa Dar es Salaam wenye
asili ya wilayani Handeni, mkoani Tanga, pamoja na maswahiba zao, wamepanga
kukutana Ijumaa ya Februari 8, katika Viwanja vya Leaders Club, kuanzia saa 10
za jioni ili kutafuta namna ya kusaidia watu wasiojiweza wilayani humo.
Kikao hicho ni cha kwanza kufanywa
na watu wa asili ya Handeni, katika jiji hili ambalo wananchi wengine kutoka
mikoa na wilaya mbalimbali wamekuwa wakikutana na kujadili hali ya maisha
inayowakabili.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, mmoja wa wajumbe wanaoandaa kikao hicho, kilichopewa jina la ‘Handeni
Kwetu’, Kambi Mbwana, alisema kwamba kukutana kwa wadau hao ni sehemu maalum ya
kutafuta namna pia ya kusaidiana na viongozi wao kwa ajili ya maendeleo yao.
Alisema kwamba Wilaya ya Handeni
imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya kila aina, ikiwamo njaa na shida ya maji,
hivyo kwa wananchi hao kukutana pamoja, wanaweza kupata ufumbuzi katika baadhi
ya mambo.
“Wakati Handeni ikiendelea kutajwa
kama wilaya zisizokuwa na maendeleo kwa miaka 51 ya Uhuru, sisi tunakutana na
kutoa kauli moja yenye tija kwa watu wote.
“Bila kuangalia nafasi zetu,
vipato vyetu au heshima katika jamii, naamini moyo tu wa kukaa na kuzungumza au
kuimba wimbo mmoja wa maendeleo, naamini mambo yatakuwa mazuri, hasa pale
kitakapofanyika kilichojadiliwa na wote,” alisema.
Handeni, inayoongozwa na Muhingo
Rweyemamu kama Mkuu wa Wilaya na Mbunge wake Abdallah Kigoda, imetajwa kukumbwa
na baa la njaa na kulazimika baadhi ya wakazi wake kulalia mboga mboga pamoja
na shida ya maji, jambo linalohitaji kujitolea kwa kila mmoja kwa nafasi yake.
Mawasiliano, +255712053949, +255753806087
barua pepe ni kambimbwana@yahoo.com
No comments:
Post a Comment