Sherehe za kutangaza vivutio vya asili vya bara la
Afrika zinategemea kufanyika katika hoteli ya Mt Meru katika jiji la Arusha
Tanzania Februari 11, 2013 kuanzia saa nane mchana.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Utalii
Tanzania viongozi mbali mbali wa kitaifa na kimataifa ambao wanatarajiwa
kuhudhuria sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.
Rais wa Taasisi iliyoendesha shindano hilo la
kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder Dr Philip Imler kutoka
Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari kutangaza vivutio Saba
vya Asili vya bara la Afrika.
Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu vilivyoingia
kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro
na wanyama wanaohama wa Seregeti. Tanzania imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa
washindi ambao angalau kivutio kimoja ama zaidi Saba ya Asili
Afrika.
Macho na masikio ya watanzania ni kujua ni kivutio
au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.
No comments:
Post a Comment