Michael Wambura
Na Kambi Mbwana,
Dar es Salaam
ALIYEKUWA
Mgombea wa Nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kabla ya
kuenguliwa na Kamati ya Uchaguzi na ile ya Rufaa, Michael Wambura, amezishukia
Kamati hizo pamoja na Katiba nzima inayosababisha utendaji mbovu wa Shirikisho
hilo na kuzitaka zitenguwe uamuzi wowote uliosababisha mkanganyiko huo.
Wambura
alienguliwa sambamba na aliyekuwa mgombea nafasi ya Urais wa TFF, Jamal
Malinzi, ambeya kwa pamoja wameleta mtikisiko mkubwa katika nyanja ya mpira wa
miguu hapa nchini, ikiwa ni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa TFF uliopangwa kufanyika
Februari 24.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo mchana, Wambura alisema Katiba ya TFF inayotumika sasa
imepitishwa kimakosa, kutokana na kuamuriwa na mtu mmoja, bila kupigiwa kura na
Kamati ya Utendaji ya TFF, sambamba na kukiukwa kwa mambo mengi.
Alisema kuwa
Rais wa Shirikisho hilo, Leodgar Tenga, amedanganya umma kwa madai kuwa Katiba inayotumika
sasa, baada ya kubadilishwa imepitishwa kihalali, wakati kanuni zake zimeanza
kutumika Januari 15, mwaka 2012, wakati Katiba yenyewe imepitishwa Januari 7
mwaka 2013, jambo ambalo linaleta mkanganyiko wa aina yake.
“Haya ndio
matatizo yaliyosababisha kuleta mkanganyiko mkubwa, hivyo bila hata kuangalia
matokeo yangu, naomba TFF, chini ya Rais Tenga kutengua uamuzi wowote wa Kamati
ya Uchaguzi na ile ya Rufaa, pamoja na kutumia Katiba ya zamani, kwasababu
waliotoa uamuzi huu wamefanya hivyo kwa sababu ya kuwashughulikia watu
wachache, akiwamo Malinzi.
“Katiba ya sasa
haijapitishwa kihalali kwakuwa Kamati ya Utendaji haijakutana na kilichopo sasa
ni kufanganya tu, huku uamuzi ukifanywa kwa ajili ya kufurahisha upande mmoja,
jambo ambalo hakika sitakubaliana nalo hata kidogo,” alisema Wambura.
Akielezea sakata
lake la kupeleka mambo ya soka mahakamani, Wambura alisema mwaka 2004, Sunday
Kayuni, aliishtaki TFF katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesi namba 21,
lakini leo hii ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho hilo.
Alisema katika
sakata hilo, anashangaa wadau wanaangalia zaidi yeye, jambo ambalo bado
hakubaliani nalo na lazima haki itendeke kwa kuvunja uamuzi wowote uliotolewa
na Kamati ya Rufaa, kwa madai kuwa imelenga kufanya kazi kirafiki, hasa kwa
Mwenyekirti wa Kamati ya Rufaa, Idd Mtinginjola, aliyekuwa swahiba mkubwa wa
mgombea wa sasa, Athumani Nyamlani.
Kwa mujibu wa
Wam bura, TFF inapaswa kusimamisha matumizi ya Katiba inayotumika kwakuwa sio
halali ili kuondoa uwezekano wa kutafutwa haki kwenye Mahakama kiraia, pamoja
na kuyafuta maamuzi yoye na kuivunja Kamati ya Rufaa.
Aidha, Wambura
alisema kwamba sifa ya mtu kuwa mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Uchaguzi
anapaswa kuwa Mwanasheria, jambo ambalo mwenyekiti wa kamati hiyo, Deogratius Lyatto,
jambo linaloifanya Kamati hiyo ikose uhalali pamoja na uamuzi wowote
unaochukuliwa na watu hao, hiyo ni kwa mujibu wa Ibara ya 49 (4).
1 comment:
wambura awapishe wenzake wafanye kazi.Suala la urafiki wa mtinginyola na Nyamlani linahusiana nini na pingamizi alilowekewa Nyamlani?AU TUAMINI KWAMBA YEYE WAMBURA NDIYE ALIYEWEKA PINGAMIZI HILO?hoja ilikuwa Nyamlani ni mtumishi wa mahakama hivyo haruhusiwi kugombea TFF,LAKINI SHERIA GANI INAYOMZUIA?KIKAO KIMEPITIA SHERIA YA UTUMISHI WA MAHAKAMA HAKUNA KIFUNGU KINACHOMZUIA.Halafu aliyemwekea pingamizi Jamal Malinzi siyo Nyamlani,ni Agape Fue,sasa hayo mambo ya kusema Mtinginyola amemuondoa Malinzi kwa vile yeye alifanya kazi na Nyamlani mahakama ya Temeke Nyamlani yanatoka wapi?Hivi tukianza kukosoa maamuzi kwa misingi ya kijinga kama hii hili taifa tunalipeleka wapi?kwamba kukiwa na mshtakiwa mluteri basi hakimu hapaswi kuwa mluteri,kesi ya mkristo hakimu lazima asiwe mkristo tunakwenda wapi?
Post a Comment