Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA chaWalemavu Tanzania (TASS), kimeandaa mafunzo ya kuchambua katiba iliyopo kwa wanawake ambao ni Albino ili kuweza kuwajengea uwelewa wa kuijua katiba hiyo na kuweza kutoa maoni yao katika Tume ya mabadiliko ya katiba mpya.
CHAMA chaWalemavu Tanzania (TASS), kimeandaa mafunzo ya kuchambua katiba iliyopo kwa wanawake ambao ni Albino ili kuweza kuwajengea uwelewa wa kuijua katiba hiyo na kuweza kutoa maoni yao katika Tume ya mabadiliko ya katiba mpya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Elnest Kimaya, alisema mafunzo hayo yameandaliwa kupitia Idara ya wanawake uzazi na watoto wa chama hicho kushirikisha wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam.
Kimaya alisema lengo kubwa la kuendesha mafunzo hayo ni kuweza kuwakutanisha wanawake hao na kuichambua kwa pamoja katiba iliyopo na kuweza kubaini kasoro, na kuweza kuwasilisha maoni yao kwenye tume hiyo ya mabadiliko ya katiba mpya.
“Walemavu wangozi tumenyimwa fursa katika katiba hii na haikutamka namna ya kuweza kuwasaidia walemavu bila kujali aina ya ulemavu sasa hapa tupo kwa ajili ya kuchambua kipengele hadi kipengele na baadae tutapata cha kuwasilisha kwa tume ya mabadiliko ya katiba.”alisema
Naye
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivukoni ambaye alikuwa mgeni rasimi
katika ufunguzi huo, Gasper Makame alitoa wito kwa watu hao wenye
ulemavu kutumia fursa hiyo ya mafunzo, iwe chachu ya kujielimisha,
kuweza kupata kitu ambacho wangependa kiingie katika katiba mpya ijayo.
“Ni fursa pekee kwenu kuweza kutumia mafunzo haya katika kuwa wa wakilisha wa akina mama wengine ambao hawakupata fursa hii ya kuhudhulia mafunzo haya na bila shaka ni haki yenu ya msingi kutoa maoni yenu kwenye Tume.”alisema Makame.
Katika hatua nyingine aliwataka wanawake hao kutumia nafasi hiyo ikiwa moja ya haki yao ya msingi kuchangia kwa njia ya maandishi maoni ya katiba mpya, lakini pia kwenda kutoa elimu watakayoipata kwa wanawake wengine ili kutetea haki zao na kuzilinda.
Kwa upande wake, Katibu wa Idara hiyo ya wanawake Mzawa Jagame, alisema fursa hiyo waliyoipata watahakikisha wanaitumia vizuri ili kuweza kuwasilisha maoni yao kwenye Tume , ikizingatiwa kuwa katiba iliyopo haikutaja namna ya kuweza kumasaidia mwanamke mlemavu na hasa albino.
Pia alitoa wito kwa wanawake walemavu kuweza kuendelea kujitokeza katika kutoa maoni yao kwenye tume ya katiba kwa njia ya maandishi ili mwisho wa siku walemavu kupata ukombozi wa kikatiba na kupata fursa katika nyanja mbalimbali.
No comments:
Post a Comment