TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF KUFANYIKA MACHI 7 NA 8 JIJINI DAR ES SALAAM
JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI KWA
WATUMISHI WA UMMA
(PSPF)
TAARIFA KWA
UMMA
Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF) unawajulisha kwamba Mkutano Mkuu wa wadau utakaofanyika
tarehe 07 na 08 Machi 2013 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni
katika Ukumbi wa JB Belmont uliopo ghorofa ya 6 ya Jengo la Maegesho la PSPF -
Golden Jubilee Towers , Dar es Salaam.
Madhumuni ya Mkutano huu ni
kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na
changamoto zinazoukabili Mfuko na Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.
Tafadhali thibitisha
ushiriki wako kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Makao Makuu, Dar es Salaam au Ofisi za
PSPF mikoani kabla ya tarehe 05 Machi 2013.
“PSPF - Tulizo la
Wastaafu”
Kaimu Mkurugenzi
Mkuu
Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma,
Golden Jubilee Towers,
Ghorofa ya 6-13, Mtaa wa Ohio/Kibo,
Central Area, Kiwanja Na.
8, 9, 12 na 15, S. L. P 4843. Dar-es-Salaam.
Simu: +255 22 2120912/52 au
+255 22 2127375 /6
Nukushi: +255 22
2120930.
No comments:
Post a Comment