Waziri wa Nishati na Madini Mh. Sospeter Muhongo
alipata fursa kuongea na Watanzania waishio Uingereza katika mwaliko rasmi
kutoka serikali ya Uingerza. Katika ziara yake nchini Uingereza Mh Sospeter
Muhongo ameambatana na Bw. Athanas Macheyeki, Bw. Seleman Hatibu na Bw.
Sosthenes Massola.
Mh. Muhongo aliwaeleza Watanzani suala zima la gas
na jinsi gani serikali itavyotumia gas hiyo kuleta maendeleo ya nchi. Amesema “serikali
itahakikisha kuwa kila kijiji kinapata umeme na mpaka kufikia mwaka 2025 nchi
ya Tanzania itaondoka na umasikini”.
Aliendelea kusema kuwa bila ya umeme
hatutoweza kutoa umasikini hivyo wizara yake itatafuta miundo mbinu ya kisasa
ili kuwezesha suala zima la matatizo ya umeme linaondoka. Pia amesema wizara
yake itaangalia tena ufumo wa Tanesco na kuanzisha idara zingine ambazo
zitashirikiana na zitawezesha kutatua matatizo yanayoikabili Tanesco.
Vilevile Mh Muhongo aliwataka wawekezaji wa Kitanzania
waweze kuwekeza katika sekta ya nishati na madini.
Habari na Ally Muhdin- London
|
No comments:
Post a Comment