Mbwana Samatta
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Washambuliaji
wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanatarajia kutua
nchini kesho (Februari 3 mwaka huu) tayari kwa mechi ya Cameroon
itakayochezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Samata
na Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo (DRC) watawasili saa 11.10 jioni kwa ndege ya PrecisionAir na
kwenda moja kwa moja kambi hoteli ya Tansoma.
Wachezaji
wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanaanza
kuripoti kambini leo jioni (Februari 2 mwaka huu) mara baada ya mechi
kati ya Yanga na Mtibwa Sugar.
Mechi
hiyo iliyo katika Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) pia itatumika kwa ajili ya kutoa ujumbe wa vita dhidi ya Malaria
viwanjani, ugonjwa unaoongoza barani Afrika kwa kusababisha vifo vya
watoto na wajawazito.
TFF
kama ilivyo Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA), Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na FIFA imekuwa
msitari wa mbele katika kueneza kampeni ya vita dhidi ya Malaria
inayoongozwa United Against Malaria (UAM). Rais wa TFF, Leodegar Tenga
na nahodha wa Cameroon, Samuel Eto’o ni miongoni mwa mabalozi wa vita
dhidi ya Malaria barani Afrika.
No comments:
Post a Comment