Kenneth Asamouh
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA) limesema linapeleka rasmi madai ya mchezaji wa zamani
wa Yanga, Kenneth Asamoah kwenye chombo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute
Resolution Chamber) baada ya klabu hiyo kutojibu chochote.
Awali FIFA ilipokea
malalamiko ya Asamoah kuwa anaidai Yanga dola 5,000 za Marekani ambapo ilikuwa
ni sehemu ya malipo yake (signing fee) baada ya kujiunga na klabu hiyo.
Desemba mwaka jana FIFA
iliiandikia barua Yanga kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
ikitaka maelezo yake kuhusu madai hayo ya Asamoah, lakini hadi sasa haijajibu
madai hayo.
Kwa mujibu wa FIFA,
hatua ya uchunguzi wa suala hilo umekamilika, na sasa linapelekwa rasmi katika
chombo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber) kwa ajili ya
kufanya uamuzi.
No comments:
Post a Comment