MAMBO FULANI MUHIMU
Diamond akiwa na mpenzi wake mpya, VJ Penny
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NATUMIA fursa hii kukushukuru wewe unayependa kuifuatilia
kona hii ya 'Mambo Fulani Muhimu', ikiwa na lengo mahususi la kuchambua na kuelezea mada
za uhusiano wa kimapenzi.
Ni katika hilo, namimi najikuta nikipata hamu zaidi ya
kuendelea kuwa katika kona hii, sambamba na wewe ili kupeana hili na lile.
Hakika, katika hilo, naamini tutaendelea kuwa pamoja kwa
ajili ya kuelezama mambo hayo.
Ndugu msomaji wangu mpendwa, wapo watu hasa wanawake
hawapendi kujishughulisha. Ni
wavivu kiasi cha kuwakera waume zao.
Ni pale wanapoombwa na waume zao, wawape haki ya ndoa, huku
wao wakiwawekea ngumu. Hawataki kabisa kwa kisingizio kwamba wamechoka.
Wengine husingizia usingizi, wakitaka walale kwanza hadi
watakapoamka. Hali hiyo ni mbaya sana. Maana wanaume ndio huwaumiza zaidi.
Wao wanapotaka haki hiyo ya ndoa, huwa wameshafika hisia,
jambo ambalo kwakweli ni gumu. Kwa bahati mbaya, akina mama hao wanaosema
kwanza walale, hawawezi kuamka wenyewe hadi watakaposumbuliwa upya.
Hii ni mbaya kwakweli. Inawatesa na kuwasononesha wenzao,
ndio maana baadhi yao huchoka hivyo kuamua suluhisho pekee ni kuwa na wapita
njia.
Wale ambao hawataki waambiwe, maana wanajua fika njia ya
kwanza ya kumteka mwanamume ni kumlaghai, kumpa raha ya ndoa hadi
achanganyikiwe.
Nafikiri hili ni jambo ambalo tunatakiwa tuliangalie upya
katika hali ya kuboresha ndoa zetu ama uhusiano wetu. Jua kabisa mikono yako
ndio inayoweza kuvunja ndoa yako ama uhusiano wako kwa mwenzako.
Huna budi kuwa makini kwa nia ya kuhakikisha kwamba ndoa
yako inaendelea kuchanua na sio kusambaratika kwa ujinga wako unaosumbuliwa na
uvivu.
Baadhi yao hujikuta wakisema, “nimechoka bwana ngoja kwanza
nilale hadi nitakapoamka,” Kauli hii ni nzuri kwao, ila ni mbaya kwa wenzao.
Hasa inapotolewa kila siku, kama njia ya kumnyima mwenzake
haki ya ndoa. Nasema haki ya ndoa kwa wale waliobarikiwa na Mungu juu ya jambo hilo.
Sawa, dini imeruhusu kwa wale walioingia kwenye ndoa, hivyo
sidhani kama yupo mwanamke ambaye anaweza kukataa tu ali mradi amkomowe mume
wake.
Hiyo siyo tabia nzuri hata kidogo. Mnapokerwa na tabia mbaya
ya uhuni wa wanamume wenu, pia mcheze kwenye nafasi zenu kwa kuziba ufa huo wa
umalaya.
Mwanamume asiyetosheka kwa mke wake, hakika ana nafasi kubwa
kutoka nje ya ndoa. Huo ndio ukweli. Wewe ambaye hii ni tabia yako kuwa makini.
Unapaswa kujua kiasi gani mtu wako anahitaji dozi zako, ndio
maana ameamua kuwa na wewe. Na kama hutaki tena, mpe sababu za kueleweka,
lakini sio usingizi.
Huo ni umbea. Usingizi unakujaje katika dimbwi hilo la
mahabati. Acha hizo wewe. Nani anaweza kusinzisia hapo? Labda wewe, lakini
mwenzako hawezi kulala, eti kwasababu wewe umemwambia ulale kwanza.
Yeye atalala macho. Akikusubiria uinuke ili umpe haki yake
ya ndoa. Wasi wasi ni kwamba kuna siku utainuka, wakati yeye ameshawasha gari
na kwenda kwa madada poa wanaojiuza ili apumzishe maumivu yake.
Utajisikiaje utakapoletewa magonjwa ya zinaa kwasababu ya
ujinga wako? Jiulize mwenyewe, maana hakika wewe ni tunu ndio maana mwanamume
wako ameamua kuwa na wewe, hivyo lazima uwe makini.
kambimbwana@yahoo.com
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment