Michael Richard Wambura
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa zamani wa kilichokuwa Chama Cha Soka nchini
(FAT) (TFF), Michael Wambura, anatarajia kutoa tamko lake leo saa sita kamili
za mchana, katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo juu ya kuenguliwa kwake
kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, katika Uchaguzi
uliopangwa kufanyika Februari 24.
Wambura ameendelea kung’ang’aniwa na wadau wa soka, kwa
kumtoa kila anapojaribu kuwania nafasi yoyote katika medani ya mpira wa miguu
hapa nchini, ikiwapo TFF.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Wambura alisema
kwamba anatafakari pamoja na kupokea barua kutoka TFF juu ya kumuengua kwake
kuwania nafasi ya Makamu wa Rais.
Alisema anaitumia nafasi hiyo kukaa na kupitia vifungu
mbalimbali vilivyokuwa kwenye Kanuni za TFF, kabla ya kuzungumzia mustakabali
wa soka la hapa nchini.
“Sijataka kukurupuka kutoa uamuzi baada ya kusikia kwenye
vyombo vya habari kuwa rufaa yangu haijakuwa nzuri baada ya matokeo yale yale
ya Kamati ya Uchaguzi kujirudia.
“Naamini nipo tayari leo mchana kuzungumzia yote kwa nia ya
kutoa picha kamili ya matokeo ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa TFF utakaofanyika
Februari 24,” alisema.
Katika Uchaguzi huo, nafasi pekee ya Urais imebaki kwa
mgombea wake, Athumani Nyamlani, baada ya mpinzani wake, Jamal Malinzi naye kutupwa
na Kamati ya Rufaa kwa madai hana uzoefu.
No comments:
Post a Comment