Wakati wadau mbalimbali wakiendelea kujitokeza
katika vyombo mbalimbali vya habari wakionyesha kutoridhishwa kwao na wakipinga
waziwazi maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF
ya kumuengua aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa shirikisho la soka nchini
Jamali Emily Malinzi, naye naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Amos
Makala amejitokeza kupinga maamuzi hayo akisema haki
haikutendeka.
Akiongea moja kwa moja katika kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Clouds FM akiwa jimboni kwake
mheshimiwa Makalla amesema maamuzi ya kamati rufaa ya uchaguzi iliyo chini ya
Iddi Mtingijola yamemshitua sana hasa kutokana na sababu zilizo elezwa hususani
juu ya sifa ya uzoefu wa miaka 5.
Makalla amesema maamuzi ya kamati hiyo yana ashiria
kutaka kuwandosha watanzania katika mapenzi yao katika soka kama ambavyo imekuwa
ikionekana katika siku za hivi karibu ambapo Tanzania imeanza kujenga upya mpira
wa miguu na tayari timu ya taifa ikianza kupata matokeo mazuri dhidi ya vigogo
wa soka barani Afrika kama Zambia na Cameroon.
Naibu waziri huyo akizungumza kama mdau wa michezo
nchini huku akijinasibu kuwa yeye bado ni mchezaji akiwa nahodha wa timu ya
bunge la jamhuri ya muungano, amemtaka Rais wa TFF Leordigar Tenga kuaangalia
upya juu ya maamuzi ya kamati yake yasije yakawatoa watanzania katika mapenzi ya
soka wakati huu ambapo Rais wa nchi Jakaya Mrisho Kikwete amekuwa akijitahidi
kuhakikisha michezo inakuwa nchini.
Jana kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF ilitangaza
kumuondoa Jamali Malinzi katika kinyanyiro cha kuwania uongozi ndani ya
shirikisho hilo kwa nafasi ya Rais kutoka na kukosa sifa ya uzoefu wa uongozi wa
michezo kwa kipindi cha miaka 5 mfululizo, baada ya kukatiwa rufaa na mdau mmoja
wa michezo aliyejulikana kwa jina la Agape Fue.
Agape pia ndani ya rufaa yake alihoji juu ya sifa ya
uadilifu wa Malinzi akitumia kigezo cha mgombea huyo kupinga waraka wa TFF wa
zoezi kupiga kura mabadiliko ya katiba ukiwa ni mwongozo wa moja kwa moja kutoka
FIFA ambao walimtaka mwanachama wake kufanya mabadiliko ya katiba yake kwa
kuingiza kipengele cha kuundwa vyombo mbalimbali kama ilivyokuwa kamati ya rufaa
ya uchaguzi, jambo ambalo hapo kabla Jamali Malinzi
alilipinga.
Malinzi
ameenguliwa kwa kukosa sifa kupitia vifungu vya katiba sehemu ya uchaguzi ibara
9(3) kifungu namba 29, 39(3) na 12(b)(d) hivyo rufaa dhidi yake iliyokatwa na
Agape Fueyake imeshinda.
No comments:
Post a Comment