Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio
pamoja na kukipiga faini ya sh. milioni 5. kwa Clouds FM na kufuta Kipindi cha
Jicho la Ng'ombe mara moja kwa kukiuka maadili ya utangazaji.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya, ikiwa ni uamuzi mkali
kwa ajili ya kuvifanya vituo vya redio kujiendesha kwa kufuata utaratibu
uliowekwa.
Vituo hivyo
Imani FM cha Dar es Salaam na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza kwa kosa la
kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya
utangazaji.
Kituo cha
Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu
na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa uchinjaji
wanyama kwa Waislamu na Wakristo mkoani Geita.
No comments:
Post a Comment