Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa bendi ya Extra
Bongo, Next Level, Ally Choki, ametangaza kuunga undugu na timu ya Villa Squad
ya Kinondoni na kuapa kufanya nayo kazi kwa ushirikiano.
Akizungumza juzi usiku katika
onyesho lao kila Jumapili linalofanyika katika viwanja vya Garden Breeze,
Magomeni, Choki alisema atasaidiana na Villa Squad katika majukumu yao ya
kimichezo.
Alisema ingawa Villa wao ni
wana soka, lakini haiwezi kuwatenganisha kwa namna ama nyingine, hivyo
mashabiki wa bendi yake wanapaswa kuunga undugu huo kwa pamoja.
“Nikiwa kama Mkurugenzi wa
Extra Bongo, napenda kusema kuwa tutakuwa pamoja na wenzetu wa Villa Squad kwa
namna moja ama nyingine, hivyo tudumishe undugu wetu.
“Hawa ni wenzetu kwa sekta ya
mpira wa miguu na sisi tunafanya muziki, hivyo naomba tuendelee kuwa pamoja kwa
kushirikiana pia katika hali ya kuleta mafanikio zaidi,” alisema.
Extra Bongo ni miongoni mwa bendi
zinazofanya vyema katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, ambayo katika
bonanza lake la Garden Breeze Magomeni, limekuwa likajaza watu wengi.
No comments:
Post a Comment