Na Mwandishi Wetu, USA
MWIMBAJI
maarufu duniani mwenye maskani yake nchini Marekani, Rihanna, amejikuta
akimmwagia sifa mpenzi wake, Chriss Brown kwa madai kuwa anavutia na
amebadilika kwa kiasi kikubwa.
Wawili
hawa walikuwa wapenzi zamani, kabla ya kuingia kwenye mgogoro mzito
uliosababisha wawe mbalimbali, ingawa sasa penzi lao limeonekana kuwa moto moto.
Raha, utamu. Ndivyo wanavyoonekana kusema, Chris Brown na Rihanna walipokuwa ndani ya Hawai Splash wakistarehe zaidi.
Rihanna
alisema kuwa hali hiyo inamfanya ajione anafaa zaidi kuwa karibu na mpenzi wake
huyo, ingawa kwa sasa wamekuwa wakitawaliwa na wivu wa aina yake, uliosabisha
kuzuka kwa minong’ono kuwa wametengana tena kwa madai kuwa Chriss alikuta
meseji za mapenzi kwenye simu ya Rihanna.
Rihanna
alisisita “Chris amebadilika kwa kiasi kikubwa huku akiwa tofauti na miaka ya
2009 alipokuwa na hasira ingawa kwa sasa tupo kwenye thamani kubwa zaidi,”
alisema.
Mwanadada huyo mwenye mvuto wa aina yake aliendeleza kummwagia sifa kwa kumuita Chris kuwa ni mwanaume mzuri na kutangaza upendo wa aina yake juu yake.
No comments:
Post a Comment