Na Adam Malinda,Dar es salaam.
KUPITIA mtandao wa Handeni kwetu ningependa wale wote
wanaoamini kuwa kusaidia ndugu zao na jamii inayosurubika katika wilaya ya
Handeni kuhusu njaa na ukame wa muda mrefu, wamesaidia kwa kumuamini mwenyezi mungu
kwa imani zao , watakuwa wamefikiri jambo la busara.
Umefikia wakati tukumbushane, tuone umuhimu wa kujenga
mapenzi ya kweli na nyumbani kwetu, tusifikiri kuwa wanasiasa tukiwaachia ni
wajibu wao kuleta maendeleo, lakini pia wajibu huenda pamoja na haki, nasi ni
haki yetu kuguswa na shida mbalimbali za nyumbani hususan sekta za afya, elimu,
kilimo na miundombinu.
Nasema haya kwa sababu viongozi tunaowachagua si malaika wa
kuweza kufanya kila jambo, muda mwingi tumeutumia kuwalaumu, ni kweli
walipoomba nafasi ya kuitumikia jamii walifahamu kuwa hawana uwezo wa kamaliza
kila shida za wananchi ,lakini waliahidi, hivyo ni haki yao kualaumiwa, je
tangu tuwalaumu tumeongeza tatizo ama tumeweza kupata ufumbuzi kwa kuwalaumu.
Njia pekee ya kujali kero za Handeni ni kujiunganisha na
kuwa na nguvu ya pamoja ili Handeni
kwanza madaraka na vyeo baadae, hii itatusaidia kuondoa wingu zito la kasi
ndogo ya maendeleo linaloikabili eneo la wilaya yetu.
Haisaidii kumlaumu mbunge, kwa kuwa aliyoyafanya ndipo uwezo
wake ulipoishia, tusimlazimishe ng’ombe kuota mapembe kama ya nyati ilhali
umbile lake na hulka viliishia hapo, tuone tunaweza kufuga mnyama gani mwenye
mapembe tunayoyahitaji, yanayoweza kutoboa mibuyu.
Lakini aina ya mapembe tunayoyataka yatategemea lishe bora
tunayompa, maana kiongozi bora ni yule mwenye kuwa na ushiriki wa karibu na
wananchi wake,kauli nzuri, ushirikiano, kujuliana hali ya mazingira husika na
kuona kinachoweza kusaidia kuondosha tatizo.
Nasema kauli mbiu iwe Handeni kwanza kwa sababu huwezi kuwa
unaguswa na kuzorota kwa maendeleo bila kushiriki kuonesha njia ya kufufua
maendeleo, njia ya kwanza wana mtandao mjue ni mshikamano wa dhati toka
mioyoni, kuendesha makongamano na vikao vya kujadili mustakabali wa Handeni .
Mfano sasakuna njaa katika maeneo mengi ya wilaya hii na
majirani zao, lakini jitihada gani zimechukuliwa na mamlaka husika, je sisi
kama wana handeni tumejipanga vipi kuunga mkono jitihada hizo, hii ni
kudhihirisha tunafuatilia kwa karibu masuala yanayogusa nyumbani.
Aidha tujitathimini wenyewe kwa kujiuliza kila hatua moja
unayoifanya ama kuchangia mjadala kuhusu Handeni unafikiri kwa ajili ya
kumfurahisha mdau wako, unalinda maslahi ya mtu, ama hulka yako ni unafiki.
Tukubaliane kuwa Handeni tatizo lipo, haliwezi kumalizwa kwa
njia ya kujipendekeza, halitafuti nani atakuwa maarufu, bali tuungane kwa
pamoja kwa ajili ya kuona kila mmoja anakuwa mchangiaji kwa namna moja ama
nyingine kuhakikisha jamii yetu inapambana na tatizo la njaa, ukosefu wa maji
safi na salama, afya zikiwemo zahanati, na shule zenye sifa ya kuitwa shule ili
ipatikane elimu bora si bora elimu.
Kuwavisha watoto wetu wakafanana, wanapendeza, bila kuwa na
majengo bora, walimu wenye sifa na uwezo wa kufundisha, wameandaliwa
kisaikolojia na vitendea kazi , hatuwezi
kuwa na elimu bora Handeni.
Ikiwa mama wajawazito wanatembea umbali wa kilometa kumi
kupata huduma za uzazi, bado tupo mbali
na dunia ya leo, zahanati zisizokuwa na dawa, wauuguzi wa kutosha vifaa
tiba duni, bado tutakuwa na mzigo mbele ya huduma za afya inayostahili.
Kama kilimo cha jembe la mkono ni kipaumbele cha serikali ya
wilaya, njaa itakuwa imeweka kambi Handeni, lazima tuhakikishe makundi ya rika
la kati na vijana wanakopeshwa matrekta kwa ajili ya kulima mashamba makubwa ya
mazao ya chakula na biashara, hali itakayowezesha kilimo kuwa na tija na
kuwavutia vijana vijijini , kuwaondoa woga wa kilimo cha jembe la mkono.
Lakini ni vizuri kufanya upembuzi yakinifu katika kuona
matrekta hayo yanakuwa ya aina tofauti, kwani maeneo mengi ya Handeni yanahitaji
kwanza matrekta ya kung’oa miti na visiki ndipo yaingizwe matrekta ya kulimia.
Sasa Handeni imepewa wawekezaji wa madini, milima yote
inayoonekana imekuwa katika himaya ya wawekezaji wazawa na wageni, bila
kujipanga Handeni inaweza kuwa shamba la bibi, wazawa wakibaki kuwa masikini wa
kutupwa, wageni wakizoa mali kwenda nazo makwao .
Tunasikitika kuwa baadhi ya vigogo waliopo serikalini na
vibaraka wao wameanza kampeni za kukomesha kauli za kudai haki kupitia magazeti
, ili wana handeni wakose pa kusemea, yaani wanajaribu kutuziba midomo, lakini
tunaamini hawataweza, wanajaribu kuziba shimo la panya kwa mkate.
Kwa ujumbe huu naomba wanamtandao mfahamu haki haiwezi
kutolewa kirahisi, haki hudaiwa kwa nguvu, muda wa kuwaacha wafanye wanavyotaka
umekwisha, kama wanataka amani iwepo Handeni, wakubali kukaa pamoja na
kujadiliana matatizo ya Handeni, lakini kama wanaendelea kuwa na makundi yao ya
kipambe kwa ajili ya kuididimiza Handeni, hatutakubali kamwe, Cuba ilikombolewa
na wanajeshi 7 wakiongozwa na Fildel Castro, wengine wengi walipoteza maisha
katika jitihada za kuleta ukombozi wa kweli.
Wana handeni mashariki-magharibi, kusini-kaskazini, kwetu ni
bora kuliko kwa mwingine, ukisifia kwa mwenzio ushakuwa mtumwa, ukimpenda baba
wa mwenzio umemtukana mama yako, Handeni yetu nzuri inahitaji umoja na
mshikamano kupambana na changamoto za kudumaza maendeleo ya Handeni.
Vinohaluse hano chili habuka kwiha,chimwe mizi ,chisumka
Handeni, vinochikekala neichilo ntongo
zetu hazikwiza vyedi, kukaya kuna gumbo, wantu wagonela maizii, suwe chadya
chips na nguku, kindedi ivyo nivyo vikikalwa, hechina mbazi na kukaya, nagaa
ivyedi chidugane chifanyanye vikudamana chongeze ubala ukuleka chikegala nkande wayetu
wapate nguvu yo ukulima chani mwakani
mnungu akajalia gumbo disekuchiwia, kukaya kukataa kuna gumbo hata suwe chimwedigumbo.
Ni miye mwanankwavi samwemzundu a.k.a Samwechengo. 0716
266171/0784 587838.
No comments:
Post a Comment