Rais wa Wazee wa Ngwasuma, Nyosh El Sadaat
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
BENDI ya FM Academia,
maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, inatarajia kufanya shoo ya aina yake katika
Ukumbi wa Arcade House, Mikocheni, katika Sikukuu ya Wapendanao (Valentine
Day), inayoadhimishwa duniani kote kila Februari 14.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa bendi hiyo, Kelvin
Mkinga, alisema kwamba shoo hiyo itakuwa ya aina yake kwa kupania kuwapa raha
wapendanao.
Alisema kuwa shoo
hiyo itadhaminiwa na kupambwa na shangwe za kinywaji cha (Windhoek), inayotumia
ukumbi huo kwa ajili ya kuwapatia mashabiki burudani kali ya muziki wa dansi.
Mkinga alisema kuwa
shoo yao ni muhimu huku ikifanyika Siku ya Wapendanao na wadhamini wakiwa ni
kinywaji cha Windhoek, wakipanga kutoa zawadi mbalimbali kwa wadau na mashabiki
wao.
“Itakuwa ni shoo ya
aina yake katika ukumbi ule, hivyo naomba wadau na mashabiki wetu waje kwa
wingi kupata ladha kamili kutoka kwa waimbaji wenye mvuto mkubwa, akiwamo
Patchou Mwamba ‘Tajiri’.
“Huwa hatubabaishi
katika shoo zetu, ndio maana wadau wote wanajua kuwa Ngwasuma hakuna zaidi
katika tasnia ya muziki wa dansi nchini, ukizingatia kuwa shoo yetu na nyimbo
zetu ni moto wa kuotea mbali,” alisema Mkinga.
Nyimbo za Ngwasuma
zinazofanya vyema katika kona ya muziki wa dansi nchini ni pamoja na Otilia,
Heshima kwa Mwanamke, Vuta Nikuvute na nyinginginezo, wakiwa chini ya Rais wao,
Nyosh El Sadaat.
No comments:
Post a Comment