Mrembo wa Tanzania mwaka 2007, Richa Adhia, katikati, katika kilele cha Valentine Day, kilichoandaliwa na kinywaji cha Baileys.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANADADA aliyewahi kunyakua taji la Miss Tanzania mwaka 2007, Richa Adhia,
amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuwajali watu wengine wakiwemo
wenye mahitaji maalum kama watoto na wazee wasiojiweza kimaisha, badala
ya kusubiri maadhimisho ya Sikukuu mbalimbali, ikiwamo ile ya Wapendanao, yani
Valentine Day kwa minajili ya kufanya uzinzi.
Akizungumza wakati wa kilele cha Siku ya wapendanao iliyoandaliwa
na na Kampuni ya Bia ya Serengeti, kupitia kinywaji cha Baileys, katika viwanja
vya shoppers jijini Dar es Salaam, Richa alisema huo sio utaratibu mzuri wa
kuijali jamii.
“Siku ya wapendanao ikitumika kuongeza ari ya
kuwasaidia watu wenye mahitaji inakuwa na maana zaidi kuliko kuitumia
siku hiyo kwa mapenzi zaidi kama wanavyofanya baadhi ya watu wanaofanya
vitendo hivyo.
“Siku hii itumike kuboresha uhusiano wa wana jamii kwa
ujumla na sio kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na watu wengi,” alisema mwanadada
huyo.
Aidha, Meneja Masoko wa vinywaji vikali kutoka Kampuni ya
bia ya Serengeti Emilian Rwejuna, alisema wameamua kufanya kampeni hii ili
kuamsha ari ya kuwajali na kuwapenda watu na kuwajali kwa kwa ujumla wake.
Alisema kuwa kampuni yao kwa kupitia kinywaji chao cha
Baileys imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhamasisha na kutoa chachu na kuahidi kuendelea
na mtindo huo.
Kampeni ya msimu wa Siku ya Wapendao ulioandaliwa hiyo ulianza
Februari Mosi mwaka huu kwa kupita maeneo mbalimbali ya manunuzi ili
kuwahamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kuwanunulia wenzi wao zawadi,
ambapo kilele chake kilikuwa juzi Februari 14.
No comments:
Post a Comment