Mkurugenz wa Extra Bongo, Ally Choki
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya Extra Bongo, Next Level, imepangwa kuusindikiza
utambulisho wa bendi mpya ya Victoria Sound, unaotarajiwa kufanyika Machi Mosi,
katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni.
Mwinjuma Muumini, Rais wa bendi ya Victoria Sound
Utambulisho huo unakuja siku chache baada ya Mwinjuma
Muumini, Rais wa bendi ya Victoria Sound, kuisuka upya kwa kuwaunganisha
waimbaji wenye uwezo wa juu, akiwamo Waziri Sonyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Victoria
Sound, Hamis Mahelo, alisema kwamba mpango wa utambulisho huo upo sawa kwa
ajili ya kuwatambulisha moja kwa moja wakali wao.
Alisema wanamuziki wao wapo kwenye kiwango cha juu katika
kuwapatia burudani wapenzi wao, wakiwa pamoja na Extra Bongo, akiwa sambamba na
bendi yake ya Extra Bongo.
“Naomba mashabiki waje kwa wingi katika utambulisho wetu huo
ambao naamini ni mwanzo mzuri kwa upande wa muziki wa dansi hapa nchini,
ukizingatia kwamba ndio tunaingia rasmi.
“Naamini kila kitu kitakuwa sawa, kwa kuhakikisha maandalizi
yetu kabambe, tukiwa chini ya Muumini, akiwa ni mwanamuziki mwenye makali ya
hali ya juu katika muziki wa dansi,” alisema.
Victoria Sound, tayari imeshaandaa nyimbo kadhaa, ukiwamo
ule wa Shamba la Bibi, unaodaiwa kuwa kijembe cha Mkurugenzi wa bendi ya Twanga
Pepeta, Asha Baraka.
No comments:
Post a Comment