Michael Wambura, akisisitiza jambo, sio leo.
Na Mwandishi Wetu, TFF
Jamal Malinzi amepeta, sasa ni mgombea rasmi wa urais TFF
MATUMAINI
ya Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Soka Tanzania (FAT), sasa Shirikisho la
Soka nchini (TFF), Michael Wambura, yametoweka rasmi leo baada ya Kamati ya
Uchaguzi ya TFF, ikiwa chini ya Deogratius Lyato, kumtupa nje.
Sababu
zilizomuondoa katika mchakato huo wa uchaguzi wa ni ule ule wa kupeleka mambo
ya soka katika mahakama za kawaida, sambamba na kukosa uadilifu. Aidha,
wagombea wa Urais, Jamal Malinzi na Athumani Nyamlani wao wamepita, huku nafasi
ya Makamu wa Rais sasa ikibaki kuwaniwa na Wallace Karia na Ramadhan Nassib.
Mbali
na Wambura, wagombea wa nafasi mbalimbali ukiwamo Ujumbe wa Kamati ya Utendaji
wapatao 1o nao wametupwa nje, akiwamo mwandishi wa habari za michezo, Shafii
Dauda, aliyetupwa kwasababu za kudanganya umma baada ya kuenguliwa katika
Uchaguzi wa IDFA.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo mchana, Lyato alisema Wambura ameondolewa
katika mchakato wa Uchaguzi huo kwa madai ya siku zote, yakiwamo uadilifu na
kuwahi kupeleka masuala ya soka, klabu ya Simba, katika Mahakama za kawaida,
hivyo kujitilia gundu la kutupwa nje kila anapojaribu kuota nafasi za uongozi.
Alisema
kuwa wapinzani wake, Wallace Karia na Ramadhan Nassib, sasa wamepeta kuelekea
kwenye Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24, ambapo pia katika nafasi ya
Urais, wagombea Malinzi na Nyamlani nao wakipeta, huku Omary Mussa Nkwarulo
naye akiwekwa kando kwasababu za kukosa
ufahamu katika nafasi anayoomba ya kuwania Urais wa Shirikisho hilo.
Mbali
na matokeo hayo, Kamati ya Uchaguzi imewapitisha wagombea wa nafasi ya Bodi ya
Ligi, Yusuph Manji na Hamad Yahya Juma kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi
hiyo, huku Said Mohamed akipita kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, wakati
wajumbe waliopitishwa ni Kazimoto Miraji na Omary Khatib.
Alisema
kwa ujumla kila aliyewekwa kando katika uchaguzi ametolewa kwa kutokidhi vigezo
kwenye Kanuni na Katiba wa TFF, vikiwamo elimu, uadilifu ama mkanganyiko
ulitokea katika fomu za maombi ya kupitishwa kwenye mchakato huo.
Mbali
na Wambura ambaye ametolewa kwasababu za kupeleka soka mahakamani, lakini wapo
ambao nao wametupwa nje, akiwamo waliomba kugombea nafasi za Ujumbe wa Kamati
ya Utendaji, wakiongozwa nao Abdalla Mussa, Mbasha Matutu, Charles
Mugondo, Ayubu Nyaulingo, Nazarius
Kilungeja, Iliud Mvella,Farid Nahdi,
Hassan Hassanoo, Omary Isaac na Shafii Dauda.
“Wajumbe
waliopitishwa kuwania nafasi ya Ujumbe ni pamoja na Alex Kamuzelya, Juma Pinto,
Muhsin Said Balhabou, waliopitishwa katika Kanda ya 13, ambayo ni jiji la Dar
es Salaam, huku Davis Mosha, Khalid Abdallah, Kusianga Mohamed waliopitishwa
kwa Kanda ya 12 ambayo ni Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga.
“Wajumbe
wengine waliopitishwa kwa Kanda ya 11 ni Riziki Juma na Twahil Twaha, huku
nafasi ya kutoka Kanda ya 10 ya Mkoa wa Dodoma na Singida, wakati Kanda ya 9
ambayo ni Mtwara na Lindi ikienda kwa Athuman Kambi, Francis Kumba, Zafarani
Damoder, huku Kanda ya 8 kwa mikoa ya
Ruvuma na Njombe, ikichukuliwa na James Mhagama, Stanley Lugenge,” alisema.
Lyato
aliwataja wengine kuwa ni kutoka Kanda ya 7 ambayo ni Iringa na Mbeya, ikienda
kwa Davis Samson, John Exavery na Lusekelo Mwanjala, wakati Kanda ya 6 ilienda
kwa Blassy Mghube, Selemani Bandiho Kameya, wakati Kanda ya 5 ambayo ni Tabora
na Kigoma wametangazwa Msafiri Mgoi na Yusuph Kitumbo.
Wengine
waliopitishwa Kanda ya 4 wakiwa ni Elley Simon, Omary Ally, wakitoka mikoa ya
Arusha na Manyara, wakati Kanda ya 3 ambayo ni mikoa ya Shinyanga na Simiyu
imeenda kwa Epaphra Swai, huku Kanda ya 2 ikienda kwa Jumbe Magali, Mugisha
Garibona, Samuel Nyalla, Vedastus Lufano
hawa wakipitishwa huku wakitoka mikoa ya Mwanza na Mara, wakati Kanda 1 ikiwa
na mikoa ya Kagera na Geita na kupitishwa Kalilo Samson na Salum Hamis Umande.
Uchaguzi
wa TFF umepangwa kufanyika Februari 24, wakati ule wa Bodi ya Ligi ukitarajiwa
kufanyika Februari 22, ambapo patashika ya kuelekea kwenye tukio hilo ukizidi
kupamba moto.
Kumalizika
kwa mchakato huo wa usaili, sasa unasababisha kuweka msuguano zaidi kwa nafasi
mbili za Malinzi na Nyamlani, kutokana na mvuto wao katika soka nchini.
No comments:
Post a Comment