Albinus Felesianu kulia akimrushia ngumi mpinzani wake kushoto.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA kijana na anayeinukia kwa kasi Albinu Felesianu wa
nchi ya Namibia amepewa ofa ya kugombea ubingwa wa dunia wa Featherweight kwa
vijana walio chini ya miaka 25 unaotambuliwa na IBF.
Albinus amezoea kupewa zawadi za Christmas na siku kuu yake
ya kuzaliwa lakini hamna kilichomwandaa na mshtuko mkubwa ambao aliupata wakati
IBF ilipotangaza hivi karibuni kuwa imempatia nafasi ya kugombea mkanda wa
dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25.
Mtua ambaye anaweza kuiua furaha yake ni mmoja wa watoto wa
Nkrumah, Mghana Ishmael Ayeetey ambaye amekulia katika moja ya viunga
vinavyosifika kwa kutoa mabingwa wa ngumi wa dunia kama kina Azumah Nelson,
Joseph Agbeko na Ike Quartey.
Albinus Felesianu kulia akimrushia ngumi mpinzani wake
kushoto
Mpambano huo utafanyika katika jiji la Windhoek nchini
Namibia tarehe 29 March chini ya kampuni ya Kinda Boxing promotions ya bwana
Kinda Nangolo!
Hili litakuwa pambano la pili la ubingwa wa dunia kwa vijana
baada ya bondia Ilunga Makabu wa Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) kumtwanga
bondia Gogito Gorgiladze wa Georgia jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini
jumamosi iliyopita.
No comments:
Post a Comment