Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Kamisheni
ya Ngumi za Kulipwa Nchini TPBC inewataka mabingwa wake wote wawe wametetea
mikanda yao ya ubingwa ifikapo tarehe 30 Marchi kwaka huu ili kuepuka
kunyanganywa.
Kwa
kipindi kirefu mabingwa kadhaa wamekuwa wanakaa na mikanda bila kuitetea.
Tunataka ieleweke kuwa muda wa kukaa na ubingwa wa TPBC ni miezi sita (6) tu na
sio mwaka mmoja.
Taarifa iliyotumwa na
Imetolewa na Onesmo Ngowi, Rais TPBC ilisema kuwa bingwa wa kweli anatakiwa awe
anafuata sheria, kanuni na taraibu za ubingwa alionao na sio kujiita bingwa
wakati hufuati masharti yaliyowekwa.
Katika
kipindi hiki cha mwaka 2013 tunawataka mabondia waheshimu sheria za mikataba
wanayotiliana sahihi na mapromota. Tunataka ngumi ziboreshwe kakini pamoja na
changamoto nyingi zilizoko, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wadhamini, mabondia
wakiheshimu mikataba yao mchezo wa ngumi utakua na kuwavutia wadhamini.
Tunapenda
pia kuwaomba wenye mapenzi mema na nchi hii wajitolekeze kwa wingi ili
kushirikiana na sisi tuiweke Tanzania kwenye chati ya dunia kama zilivyo nchi
nyingine.
No comments:
Post a Comment