Boniface Wambura, Msemaji wa TFF
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAKATI Uchaguzi wa
Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), ukipangwa kufanyika Februari 14, mkoani
Morogoro, hadi sasa nafasi ya Mweka Hazina ikiombwa na mwanamichezo mmoja tu,
ambaye ni Jovin Ndimbo.
Mbali na Ndimbo,
nafasi nyingine za uchaguzi huo zinawaniwa na Army Centimeya, Said Nasoro ambao
wameomba kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa (TAFCA), Eugene Mwasamaki, alisema kwamba
wadau wengine waliochukua fomu hizo ni Juma Chaponda, Juma Mpuya na Tifika
Kambi wanayetaka nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Alisema nafasi ya
Katibu Mkuu inaombwa na Abdallah Mitole, Charles Ndagala na Hamis Kisiwa,
ambaye hawa watachuana kuitaka nafasi hiyo nyeti TACFA.
“Wengine ni Mjumbe wa
Mkutano Mkuuiliyoombwa na Kamwaga Tambwe, huku nafasi kama hiyo kwa upande wa
wanawake ikiombwa na Isabela Kapela, huku Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ikiombwa
na Samson Mkotya,” alisema Mwasamaki.
Hapo kabla, uchaguzi
wa TAFCA, ulisimamishwa na Kamati ya Uchaguzi kwa kutokidhi vigezo, hivyo
kuwaondolea sifa ya kuingia kwenye Uchaguzi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),
uliopangwa kufanyika Fabruari 24.
No comments:
Post a Comment