Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah
Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) linawataka washabiki wa mpira wa miguu kujitokeza kwa
wingi wikiendi hii kuzishangilia timu za Azam na Simba zitakazocheza mechi za
mashindano ya Afrika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo mchana,
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema kwamba Nguvu ya washabiki ni muhimu
katika kuziweza timu hizo kufanya vizuri katika mechi hizo za nyumbani dhidi ya
Al Nasir Juba ya Sudan Kusini na Club Libolo ya Angola.
Azam itacheza Jumamosi
(Februari 16 mwaka huu) dhidi ya Al Nasir katika mechi ya Kombe la Shirikisho
wakati Simba itaikabili Club Libolo kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika
itakayofanyika Jumapili. Mechi zote zitachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Aidha, Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inamaliza raundi ya 16 kesho
(Februari 13 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji African Lyon dhidi ya Yanga
itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo
itakayochezshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro inakutanisha timu
zenye mazingira tofauti. Wakati Yanga wakiwa ndiyo vinara wa ligi hiyo kwa
pointi 33, African Lyon ambayo sasa inanolewa na Salum Bausi inakamata mkia
ikiwa na pointi tisa tu.
Nayo Toto Africans
itaikaribisha Polisi ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Musoma. Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000 utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Oljoro JKT.
Nahodha wa zamani wa
Taifa Stars, Mecky Maxime ambaye sasa ni kocha wa Mtibwa Sugar ataiongoza timu
yake hiyo katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Manungu ulioko
Turiani, Morogoro. Ni kwenye uwanja huo huo ambapo Mtibwa Sugar katika mechi
yao iliyopita walichapwa mabao 4-1 na Azam.
No comments:
Post a Comment