Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SEKRETARIETI ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepokea barua ya Serikali
ikielezea uamuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella
Mukangara kutengua uamuzi wa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo nchini
kuidhinisha marekebisho ya Katiba ya TFF toleo la 2012.
Baada ya kupokea barua
hiyo jana alasiri (Februari 25 mwaka huu), Sekretarieti iliwasiliana na Rais wa
TFF, Leodegar Tenga ambaye ameagiza kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati ya
Utendaji kujadili tamko hilo.
Kikao hicho cha Kamati
ya Utendaji ya TFF kitafanyika Jumamosi (Machi 2 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
Katika hatua nyingine, Mwamuzi msaidizi wa
FIFA, Ferdinand Chacha ameondolewa kuchezesha mechi za VPL baada ya kupata
alama za chini kwenye mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa mwezi
uliopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Waamuzi wanaopata alama 6.5 au chini
ya hapo kati ya 10 zinazohitajika pia wanaondolewa kwenye mechi za VPL na FDL.
Waamuzi wengine
walioondolewa kwa kutomudu mechi walizochezesha za VPL ni Mathew Akrama (Yanga
vs Simba), Ephrony Ndissa (Yanga vs Simba), Ronald Swai (Yanga vs Mtibwa
Sugar).
Walioondolewa kwa kupata
alama za chini ni Alex Mahagi (Simba vs JKT Ruvu), Methusela Musebula (Toto
Africans vs Coastal Union), Lingstone Lwiza (Toto Africans vs Coastal Union),
Idd Mikongoti (Toto Africans vs Mtibwa Sugar) na Samson Kobe (Toto Africans vs
Mtibwa Sugar).
Masoud Mkelemi aliyekuwa
mwamuzi wa mezani katika mechi ya FDL kati ya Moro United na Villa Squad
ameondolewa kwa kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match
meeting) na alichelewa kwa dakika tano kufika uwanjani.
No comments:
Post a Comment