Aota kufanya ngoma na P
Square, Jay Dee
Msanii Saraff anayeishi Marekani mwenye uraia wa Tanzania, akiwa kwenye pozi kali la kimauzo.
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KUANZIA
miaka ya 2000 hadi leo, Tanzania imekuwa ikishuhudia wimbi kubwa la vijana wanaojiingiza
katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva.
Saraff akiwa Studio
Tangu
wakati huo pia tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika tasnia hii, ambapo vipaji
vimekuwa vikichomoza na kujipatia mafanikio ya aina yake.
Msanii Saraff akiwa kwenye pozi.
Miongoni
mwa wasanii hao ni Ashraf Omar Maundi, maarufu kama Saraff, anayefanya kazi
zake kwa umahiri na kuwa na malengo makubwa kisanaa.
Saraff
anasema kwamba alichelewa kujitokeza katika sanaa hiyo kwa kuhofia wazazi wake,
ambao alijua hawatamruhusu kufanya kazi za sanaa.
“Lakini
kwa sababu kipaji hakijifichi, nikiwa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari
ya Airwing, jijini Dar es Salaam, nilianza kujishughulisha na muziki, hasa kwa
kuandika mashairi na kuimba.
“Ndoto
yangu ilianza kufanikiwa mwaka 2005, pale wazazi wangu walipohamia nchini
Marekani nikiwa sambamba nao, ambapo nilirekodi wimbo wangu wa ‘Demu wa Kibongo’, anasema Saraff.
Msanii
huyo anasema kwamba licha ya wimbo huo kutokufanya vizuri, lakini alijifunza
mambo mengi yanayohusu muziki, ikiwa ni pamoja na kuingia katika darasa la
masuala ya muziki.
“Ilinibidi niingie darasani kidogo nikajifunza
muziki ambapo pia niliweza kurekodi wimbo
na video. Mwaka 2010 nilitoka kwenye studio yangu kwa kutengeneza wimbo
wa ‘Unanidatisha’, nilioimba kwa
kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza,” anasema.
Anasema
kuwa alifarijika kuona Watanzania na wasio Watanzania nchini Marekani, wakiupokea
vizuri wimbo wake, hivyo kuwa njia ya kumpatia mafanikio zaidi.
Mwishoni
mwa mwaka jana, alifanikiwa kutengeneza wimbo wa kwanza kama mtayarishaji na mwimbaji,
wimbo unaofahamika kwa jina la Next Flight.
“Nilikamilisha
wimbo wangu, wa kwanza ambao niliuandaa mwenyewe, nitahakikisha natumia muda
mwingi zaidi kuandaa nyimbo zangu mwenyewe, hii itasaidia kutoa vitu kulingana
na mtazamo wangu,” anasema.
Akizungumzia
soko la muziki wa Tanzania, Saraff anasema muziki unazidi kufanya vyema, ingawa
safari bado ni ndefu ili kufikia kiwango cha Nigeria, Ghana na Afrika Kusini.
“Safari
bado ni ndefu, wengi bado wanafanya kazi kwa kubahatisha, hivyo ni vigumu sana
kuingia katika soko la kimaitafa kwa mtindo huu,” anasema.
Msanii
huyo anasema kuwa yupo katika harakati za mwisho za kumalizia wimbo wake mpya wa
lugha ya Kiswahili, ambao anaamini utafanya vizuri.
“Lakini
pia katika kuboresha kazi zangu nina ndoto ya kuja kufanya kazi na Lady Jay Dee
kwa hapa nyumbani na kwa nje P Square, natamani sana na naamini itawezekana.
“Kikubwa
ninachopenda kuwaambia wasanii wenzangu ni kuhakikisha tunazidi kuboresha kazi
zetu ili zifanye vizuri ndani na nje ya nchi na kwa kufanya hivyo, tutazidi
kuwa na mashabiki wengi zaidi,” anasema.
Kwa
sasa Saraff pamoja na kujishughulisha na masuala ya muziki, yuko mbioni
kumalizia shahada yake ya kwanza katika Chuo cha York College, jijini New York,
nchini Marekani.
WASIFU:
Jina:
Ashraff Omar Maundi
AKA:
Saraff
Alizaliwa:
Januari 26 mwaka 1988.
Utaifa:
Mtanzania
Umri:
25
Fani:
Muziki wa Bongo fleva
Anapoishi:
Jimbo la Brooklyn jijini New York, Marekani
No comments:
Post a Comment