Katibu Mtendaji wa Bazara la Mitihani Tanzania, Joyce Ndalichako, akionyesha moja ya karatasi za majibu zilizoandikwa uchafu na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne hapa nchini mwaka 2012.
Na Handeni Kwetu Blog
MATOKEO mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012, yaliyotangazwa
mapema wiki hii, yamesababisha kifo cha Michael Fidelis, aliyekuwa mwanafunzi
wa shule ya Sekondari ya Kanyenye, iliyopo mkoani Tabora, baada ya kujinyonga
kwa kamba ya manila.
Taarifa za kujinyonga kwa mwanafunzi huyo aliyeacha ujumbe
wa kutofurahishwa na zero aliyopata, imemfanya asitishe uhai wake, ikiwa ni hatua mbaya.
Habari kutoka kwa familia ya Fidelis zinasema kwamba mara
baada ya mtoto wao kujua kuwa amefeli mtihani, alichukua uamuzi huo wa
kujinyonga.
Asilimia 75 ya wanafunzi wa kidato cha nne mwaka huu
wamepata zero, hivyo kuleta balaa kubwa kwa wadau wa elimu hapa nchini, huku
wengineo wakitaka Waziri wa Elimu, Shukuru Kawambwa ajiuzulu kwa kukwepa aibu
hiyo.
Pamoja na mambo mengine, matokeo ya mwaka huu yamezikumba
zaidi shule za serikali, huku watoto wa masikini ndio wakionyesha kuathirika
zaidi.
Habari hii imeandikwa kwa msaada wa Clouds FM.
Habari hii imeandikwa kwa msaada wa Clouds FM.
No comments:
Post a Comment