Na Heka, Paul, Maelezo
VIJANA
nchini wameshauriwa kutumia fedha za mikopo wanazozipata kwa ajili ya
kuanzisha biashara endelevu zitakazowasaidia kujikwamua kimaisha na
kujiletea maendeleao.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana nchini Profesa
Elisante Ole Gabriel kutoka Wizara ya Habari ,Vijana,Utamaduni na
Michezo wakati akitoa elimu kwa vijana wajasiliamali wa manispaa ya
Kinondoni,Temeke na Ilala ,jijini Dares Salaam ikiwa ni ziara yakr ya
muda wa siku mbili iliyoanza leo.
Alisema vijana yoyote ambaye ni mjasiriamali anatakiwa kuwa na uwezo
na uwelewa wa kuendesha mradi huo pamoja na kuzitambua changamoto
atakazokumbana nazo wakati shughuli zake.
Profesa Gabriel alisema kuwa ni muhimu kwa kila mjasiriamali kijana
anaetaka kuanzisha mradi kufanya biashara halali ambayo inakibali na
pamoja na kujua namna ya kupanga bei ya biashara zake.
Aliongeza kuwa ipo mihimili mitatu ya maendeleo ya biashara ambayo
vijana wenyewe, serikali ambayo inatakiwa kuweka mfumo mzuri kwa ajili
ya shughuli za maendeleo ya vijana pamoja na kuwepo kwa wadau wengine
wa maendeleo.
Profesa huyo alizitaja gharama tatu za msingi katika kuanzishia mradi
ambazo ni lazima kuwepo na malighafi, watumishi na uangalizi wa mradi
huo.
Aliwataka vijana pia kuepuka kubaguliwa au kubaguana kwa kupitia mlango
wa siasa, dini na kikabila wanapoendesha shughuli zao za ujasiriamali.
Naye Afisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Ananias Kamundo
alisema kuwa ni muhimu kwa kila mjasiriamali mwenye biashara yoyote
ambayo ni halali kuifungulia leseni ambayo mjasiriamali malipo na lazima
awe na namba ya mlipa kodi ambayo ataipata Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA)pamoja na kitambulisho kitakacho mtambulisha kuwa ni raia wa
nchini.
No comments:
Post a Comment