Katibu Mkuu TASWA, Amiri Mhando
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
kimefuta wazo la kuendesha mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu za
uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Akizungumza na Handeni Kwetu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TASWA,
Amir Mhando, alisema kuwa mdahalo huo ulikuwa ufanyike Februari 15, 2013 na
tayari chama kilikuwa katika hatua nzuri ya mazungumzo na wadhamini pamoja na
kituo kimoja cha televisheni kwa ajili ya kurusha 'live' tukio hilo, ambapo
kesho ilikuwa tutangaze utaratibu mzima wa mdahalo huo.
Alisema katika mazungumzo ya leo na uongozi wa kituo hicho
ambao hautaki tukitangaze, tumekubaliana kufuta wazo la mdahalo kwa
sababu nafasi ya urais amebaki mgombea mmoja, hivyo mdahalo hautakuwa na tija.
“Dhamira ya awali ya kufanya mdahalo ilikuwa kuwapa fursa
wapiga kura wasikie vyema sera za wagombea urais na Makamu wa Rais, ili
wananchi wawasikilize wagombea hao na pia wapiga kura wawatambue vizuri.
“Hata hivyo TASWA itatafuta utaratibu mwingine mzuri ambao
utawezesha wagombea kuzungumza na waandishi wa habari na kuulizwa maswali
mbalimbali ambayo tunaamini kwa kiasi fulani yatasaidia wapiga kura katika
uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu,” Alisema.
TASWA imekuwa ikifanya mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu
kwenye uchaguzi wa TFF, ilifanya hivyo mwaka 2001 na mwaka 2004 ingawa haukuwa
wa live, ikafanya wa live mwaka 2008, ambapo yote ilikuwa ya mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment