Nurdin Bakari akiwajibika uwanjani.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Yanga na Mtibwa Sugar
zinapambana kesho (Februari 2 mwaka huu) katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi Ronald Swai
kutoka Arusha ndiye atakayechezesha mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na upinzani
mkali, kwani wakati Yanga ikiongoza ligi hiyo, wapinzani wao Mtibwa Sugar
katika mechi iliyopita walilala mbele ya Polisi Morogoro ambayo ni ya mwisho
katika msimamo wa ligi kwa sasa.
Polisi Morogoro itakuwa
mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro wakati Uwanja
wa Mkwakwani, jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na
Ruvu Shooting inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa.
Keshokutwa (Jumapili)
kutakuwa na mechi mbili. Simba itaumana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam huku Tanzania Prisons ikiikabili Coastal Union katika Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment