Ally Choki
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
MKURUGENZI wa bendi
ya Extra Bongo, maarufu kama Wazee wa Kizigo, Ally Choki, amesema kwamba
bonanza lao la kila Jumapili, linajaza watu kwasababu ya kuwasogezea burudani
hizo karibu.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika viwanja hivyo vilivyopo karibu na Hospitali ya Magomeni, jijini
Dar es Salaam, Choki alisema kwamba sasa mashabiki wao wameipata burudani hiyo
karibu zaidi.
Alisema kila Jumapili,
shoo yao hiyo imekuwa ikijaza watu wengi wanaokwenda kuangalia burudani kutoka
kwa waimbaji na wanenguaji mahiri, akiwamo Rogati Hega Katapila, Ramadhan
Masanja Banza Stone na wengineo wenye majina ya kutisha.
Choki alisema kwamba
kwasababu hiyo wanaamini kuwa bendi yao itazidi kufanya vyema kwa kubuni mambo
yenye kuleta tija katika maisha ya muziki wa dansi nchini.
“Sisi kama Extra
Bongo tumekuwa kwenye mikakati ya kuweza kuwavuta au kuwasogezea burudani
mashabiki wetu, hivyo naamini kwa kufanya bonanza hili la kila Jumapili, mambo
yatakuwa mazuri.
“Naomba wadau na
mashabiki waje kuangalia jinsi timu yangu ilivyojipanga kuanzia waimbaji hadi
wacheza shoo wetu wanaongozwa na Super Nyamwela,” alisema Choki.
Extra Bongo kwa sasa
inafanya vyema katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, hivyo shoo zao
zote wanazofanya katika kumbi mbalimbali kupata mashabiki wengi.
No comments:
Post a Comment